Menu

Friday, June 6, 2025

Wananchi Mkoa wa Kusini Unguja Kufurahia kwa Amani Sikukuu ya EID EL ADH-HA – RPC SHILLAH

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP.Daniel Shillah amesema Swala na Baraza la Eid linalotarajiwa kufanyika Mkoa wa Kusini Unguja Kitaifa pamoja na Skukuu ya EID EL ADH-HA zitafanyika kwa Amani na utulivu.

Akizungumza na Waandishi wa habari huko Tunguu, Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kusini Unguja amesema Jeshi la Polisi Katika Mkoa huo limejipanga kuimarisha ulinzi maeneo yatakapofanyika Baraza la Eid, nyumba za ibada, maeneo ya fukwe, kumbi za starehe na maeneo yote yatakuwa salama.

Aidha Kamanda Shillah amewasisitiza Madereva na waendesha vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani kwa kutokwenda mwendo wa kasi, kutopakia abiria kupita kiasi na kutoendesha vyombo hivyo wakiwa wamelewa.

Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari

Makao Makuu ya Polisi

Kamisheni ya Zanzibar.

05/06/2025

 

No comments:

Post a Comment