Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP.Daniel Shillah amesema Swala na Baraza la Eid linalotarajiwa kufanyika Mkoa wa Kusini Unguja Kitaifa pamoja na Skukuu ya EID EL ADH-HA zitafanyika kwa Amani na utulivu.
Akizungumza na Waandishi wa
habari huko Tunguu, Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kusini Unguja amesema Jeshi
la Polisi Katika Mkoa huo limejipanga kuimarisha ulinzi maeneo yatakapofanyika
Baraza la Eid, nyumba za ibada, maeneo ya fukwe, kumbi za starehe na maeneo
yote yatakuwa salama.
Aidha Kamanda Shillah amewasisitiza Madereva na waendesha vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani kwa kutokwenda mwendo wa kasi, kutopakia abiria kupita kiasi na kutoendesha vyombo hivyo wakiwa wamelewa.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari
Makao Makuu ya Polisi
Kamisheni ya Zanzibar.
05/06/2025
No comments:
Post a Comment