6/recent/ticker-posts

UOKOAJI KATIKA AJALI YA MV FATIH

UOKOAJI ULIOANZA USIKU NA KUENDELEA KWA SIKU YA LEO ASUBUHI MPAKA SASA HAKUNA MAITI ILIOKOLEWA ZAIDI YA ZILE TATU ZILIZOPATIKANA
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA AJALI YA MELI YA FATIH IKIWA IMEBIRUKA KATIKA BANDARI YA ZANZIBAR IKITOKEA DAR-ES-SALAAM IKIWA NA ABIRIA NA MIZIGO MPAKA SASA TAYARI MAITI TATU ZIMESHAPATIKANA USIKU WA JANA.

WANANCHI WALIOFIKA LEO ASUBUHI KUSHUHUDIA AJALI YA MELI YA FATIH WAKIWA NJE YA BANDARI YA MALINDI KUTAKA KUJUWA WATU WALIOPATA AJALI HIYO YA MELI
MWILI WA MTOTO ALIYEFARIKI
WAFANYAKAZI WA MSARABA MWEKUNDU WAKIONDOA MWILI WA MMOJA WA MAITI WA AJALI YA MELI YA FATIH

MABAHARIA WA BOTI YA RUBANI YA SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR WAKISHUSHA MIILI YA MAREHEMU WATATU WA AJALI YA MELI HIYO AKIWEMO MTOTO WA KIUME NA WATU WAZIMA MMOJA WA KIUME NA WA KIKE
WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WA KAMATI YA UJENZI NA MAWASILIANO WAKIFUATILIA UTARATIBU WA UOKOAJI WA ABIRIA WA MELI YA MV FATIH USIKU WA 29-5-2009, KUTOKA KULIA ZAKIA OMAR JUMA CUF, MZEE ALI USSI CCM,MAKAMO MWENYEKITI HAMADI MASOUD HAMADI CUF, RAMADHANI NYONGE CCM NA MWENYEKITI WA KAMATI HIYO KAMAL BASHA CCM.

KAZI NJEMA YA UOKOAJI MDAU WANGU

KAZI INAANZA YA UOKOAJI WAHANGA WA MELI YA MV FATIH
WAZAMIAJI WAKIINGIA KATIKA BOTI KWA AJILI YA KUZAMIA KUOKOA ABIRIA WALIOKUWEMO
WAOKOAJI WAKIJIANDAA KWA AJILI YA KUTOA MSAADA KAMA KUNA ABIRIA YUKO HAI KATIKA MELI HIYO YA FATIH INAYOMILIKIWA NA KAMPUNI YA SEA GULL ZANZIBAR
MAANDALIZI YA UOKOAJI WA ABIRIA YAKIANZA
MTAALAMU WA KUZAMIA KIPANDE AKIANDIKA MAJINA YA VIJANA WAKE WATAKAOPIGA MBIZI KUOKOA BAADHI YA ABIRIA NA MIZIGO ILIYOKUWEMO KWENYE MELI

Post a Comment

0 Comments