Na Khamis Amani
UPANDE wa mashitaka katika mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe, unaosimamia kesi ya kuchoma moto msahafu pamoja na juzuu za dini ya Kiisilamu, inayomkabili mkaazi mmoja wa Mombasa wilaya Magharibi Unguja, umefunga ushahidi wake katika kesi hiyo.
Hatua hiyo ya upande wa mashitaka, imekuja baada ya kumaliza kuwasilisha mashahidi wake mahakamani hapo.
Jumla ya mashahidi sita akiwemo mpelelezi wa kesi hiyo, Z 2189 Sajenti wa Polisi Suleiman wa Kituo cha Polisi Mazizini wamesikilizwa na mahakama hiyo ya inayoendeshwa na hakimu Khamis Ali Simai.
Kutokana na hatua hiyo, upande wa mashitaka ulioongozwa na Mwanasheria wa serikali Raya Issa Mselem, kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), unaipa nafasi mahakama hiyo kupitia kwa kina maelezo ya mashahidi wake, na baadae itoe uwamuzi wake mdogo (rulling).
Hivyo, kutokana na hatua hiyo, hakimu Khamis Ali Simai amelazimika kuiahirisha kesi hiyo hadi Januari 24 mwaka huu kwa kuitolea uwamuzi huo.
Chini ya kifungu cha 215 (1) cha sheria za mwenendo wa jinai (CPA) namba 7/2004 sheria za Zanzibar, mahakama hiyo itatoa maamuzi hayo dhidi ya mtuhumiwa huyo, endapo kama atakuwa na shitaka la kujibu au la.
Mtuhumiwa wa kesi hiyo ni Ramadhani Handa Tuma (28), ambaye alifikishwa mahakamani hapo Novemba 18 mwaka jana na kusomewa mashitaka hayo na Mwanasheria wa serikali kutoka Afisi ya DPP Khamis Jaffar Mfaume, ambayo aliyakana.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani hapo, ilielezwa kwamba kinyume na kifungu cha 74 (1) (b) cha sheria za Zanzibar, Novemba 16 mwaka jana alidaiwa kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani.
Mahakama ilifahamishwa kuwa siku hiyo, mahala hadharani kwa makusudi na bila ya halali alichoma moto msahafu pamoja na juzuu za dini ya Kiislam, kitendo ambacho kilidaiwa kuwa kingeweza kuleta uvunjifu wa amani kwa jamii ya dini ya Kiislamu.
Tukio hilo lilidaiwa kutokea huko Mombasa wilaya ya Magharibi Unguja, majira ya saa 2:30 za usiku.
Sambamba na shitaka hilo, pia alidaiwa kuikashifu dini hiyo ya Kiisilamu kwa kuchoma moto vitabu hivyo, kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 117 na 27 cha sheria za Zanzibar.
Mtuhumiwa huyo bado anaendelea kupumulia rumande kwa kile kilichodaiwa ni kujisalimisha na maisha yake, kutokana kitendo hicho alichodaiwa kukifanya, kimeitia hasira jamii ya Kiisilamu, na kuwepo kwake nje kwa dhamana kunaweza kusababisha madhara juu yake.
1 Comments
Natangaza sh milioni 1, ukinilietea mokono wake wa kulia huyo mtovu wa adabu wa dini yetu.
ReplyDeletesiku mtayaomtoa kichwa chake halai yetu mshenzi huyo