6/recent/ticker-posts

HUKUMU YA GHAILANI JUMAANE 25-01-2011

                                       Mama yake Ahmed Ghailani, Bimkubwa Said Abdullah
                                               Nyumba aliyokuwa akiishi Gongoni Zanzibar
Ahmed Ghailani
Benjamin Weiser, New York Times

Mwaka 2000 Usaamah bin Laden alikuwa akitembelea nyumba moja ya wageni Kandahar, Afghanistan na mmoja katika wasaidizi wake alimkaribia kijana mmoja wa kitanzania na kumwambia kwamba ameombwa na Bin Laden mwenyewe awe mlinzi wake.

Ahmed Ghailani alikubali na kukabidhiwa bunduki aina ya AK47 na kujiunga na kikundi cha watu 15 waliokuwa walinz wa bin Laden kiongozi wa al Qaaidah. Kwa mujibu wa maelelzo ya FBI kama walivyohadithiwa na Ghailani mwenyewe kwamba alikuwa pia mpishi wa Bin Laden kazi ambayo wengi wa walinzii walichukia.

Leo Jumaane ni siku ambayo Ghailani, 36, atahukumiwa katika Mahakama ya Federal District Court huko Manhattan Marekani kwa kosa la kula njama kuharibu mali za serikali kutokana na kushiriki kwake katika ulipuwaji wa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 1998. Ghailani hakukutwa na hatia kwa makosa 280 ya mauaji na kula njama katika kuua.

Mawakili wa Ghailani wanasema alikuwa kijana mdogo asiye na upeo na kughilibiwa kusaidia katika mpango huo huku waendesha mashtaka wakimwita ni gaidi na Jaji Lewis A. Kaplan alisema katika hukumu yake Ijumaa kwamba kuna ushahidhi wa kutosha kwamba Ghailani aliuwa akijua fika kinachoendelea na alishiriki mwenywe bila ya kughilibiwa.

Hata hivyo baraza la ushauri halikupata nafasi ya kuijua historia kamili ya Ghailani kabla ya Al Qaaidah wala hawakuelezwa kwa urefu na muda mwingi wa kesi yake uliangalia zaidi mahusiano yake na Al Qaaidah, kukutana kwake na Khalid Sheikh Mohammed na pia kumuona Zacarias Moussaoui.

Ukitaka habari kamili nenda kwenye link hapa chini


Post a Comment

1 Comments

  1. odosha upuuzi uliouweka hauna kichwa wala miguu ndo nyinyi nnaoshabikiya ujinga usioufahamu jee una uhakika na kinachoendeleya au unafurahiya ngoma usiyoijuwa MUUGU ATAKUSAIDIYA AKUVUWE NA HILO NA MENGINE

    ReplyDelete