Na Mwantanga Ame
MAADHIMISHO ya sherehe za miaka 34 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi wanachama wa chama hicho Mkoa wa Mjini wamepanga kufanya tathimini ya uchaguzi mkuu uliopita katika matawi yote ya Chama hicho.
Hatua hiyo ya CCCM inakuja ikiwa tayari kimeingia katika juma la maadhimisho hayo kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Februari 5, 1977 kikiwa chini ya uongozi wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi ambao walikuwa viongozi wakati wa kuviunganisha ASP na TANU.
Kutokana na kufikia umri huo CCM kimeeleza katika taarifa yake iliyoisambaza kwa vyombo vya habari na Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Mjini Maulid Issa imesema kuwa matawi ya CCM ya Wilay hiyo yataadhimisha sherehe hizo kwa kufanya tathmini ya uchaguzi mkuu uliopita.
Tathmini hiyo alisema CCM itafanyika ikiwa ni moja ya jambo la msingi kuangaliwa kwa wakati huu ikiwa pamoja na kuliangalia asuala la mporomoko wa maadili kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho na jamii kwa jumla.
Sambamba na kuliangalia hilo Katibu huyo pia alieleza mambo mengine ambayo yatatendekea katika juma hilo la sherehe ni pamoja na kuwepo makongamano yatayozungumzia historia ya kuungana kwa TANU na ASP.
vile vile alisema sherehe hizo zitazowahusisha viongozi wa juu wa Chama hicho katika kufungua matawi mapya ikiwa pamoja na kuweka mawe ya msingi katika sehemu mbali mbali za Mkoa wa mjini.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, Februari 2, 2011, anatarjiwa kuweka jiwe la msingi la maskani ya Kachorora pamoja na viongozi wengine wa Chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa Chama Mkoa Yussuf Mohammed Yussuf atashiriki katika mpira wa miguuu kati ya Halmashauri ya Wilaya, na Umoja wa vijana Dole.
Alisema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kulifungua tawi la CCM la Meya Juu Februari 3,2011 ikiwa apamoja na tawi la Kilimani Mashariki ambapo baadae atawahutubia wanachama wa Chama hicho katika mkutano wa hadhara.
Alisema katika kilele cha sherehe hizo pia Dk. Shein, atashiriki katika matembezi makubwa ya mshikamano na mkutano wa madhimisho ya sherehe za miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM katika kiwanja cha Mwembe kisonge, Michenzani Mjini Zanzibar.
Viongozi kadhaa wanatarajiwa kushiriki katika shuguli zilizopangwa na chama hicho
0 Comments