6/recent/ticker-posts

WAZANZIBARI 100 BADO WAKO SHIMONI MOMBASA KENYA

 Serikali yasema huo ni uamuzi wao

Na Salum Vuai, Maelezo

WAZANZIBARI wapato 100 bado wanaendelea kuishi uhamishoni mjini Mombasa ambako walikimbilia tokea mwaka 2000/2001.

Hayo yamethibitishwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, wakati akijibu masuali ya waandishi wa habari katika mkutano aliuandaa mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo mjini Zanzibar.


Waandishi hao walitaka kufahamu iwapo kuna Wazanzibari waliobaki katika mji wa Mombasa Shimoni, baada ya kuundwa serikali yenye mfumo wa umoja wa kitaifa.

Aidha walitaka kujua, kama wapo, serikali inachukua jitihada gani kuwashawishi kurejea nchini kuendeleza maisha na kuijenga nchi yao wakati huu ambapo kumekuwa na mshikamano mkubwa.

Makamu wa Kwanza wa Rais alisema, serikali inafahamu kuwa bado wako wananchi wapatao 100 walioamua kuendelea kuishi mjini nchini Kenya.

Alieleza kuwa, inaonekana wananchi hao wameamua kujiendeleza kimaisha huko, ingawa mara kadhaa serikali ya Zanzibar imejaribu kuwaomba warudi nchini.


"Tumefuatilia na kubaini kuwa bado wapo Wazanzibari wapatao mia moja waliobaki huko Shimoni, wengine wameshaoa na kuzaa, na wanakuja kutembea na kuondoka, yaelekea wameamua kuishi huko kwani tumekuwa tukiwanasihi kurudi bila mafanikio," alisema

Hata hivyo, alifahamisha kuwa, kama wameamua kuishi huko, huo ni uamuzi wao na wana haki ya kufanya hivyo kama ilivyo kwa wananchi wengine wanaoishi nchi za nje, na serikali haiwezi kuwalazimisha
kurudi nchini.

Post a Comment

0 Comments