6/recent/ticker-posts

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani laTaifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako Azungumza na Waandishi Zanzibar.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar matokeo ya kufutwa kwa mitihani kwa baadi ya Skuli kutokana na kufanya udanganyifu.mkutano huo umefanyika Hoteli ya Bwawani Zanzibar.  
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako, akionesha ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Uchunguzi ya Vyombo vya Usalama kuhusi undanganyifu wa baadi ya miandiko iliotumika katika mitihani ya watahiniwa wa Kidatu cha Nne.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Matihani la Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichoka, akionesho karatasi za mitihani ambozo zimekuwa na miandiko zaidi ya mmoja na kufanana maneno ya majawabu.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Dk Joyce Ndalichoka, akitowa maelezo ya kufutiwa mitihani watahiniwa wa kidatu cha Nne, wa mwaka 2011. 
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Dk Joyce Ndalichoka, akitowa maelezo ya kufutiwa mitihani watahiniwa wa kidatu cha Nne, wa mwaka 2011.


Viongozi wa Chama cha Walimu Zanzibar , wakiangalia moja ya karatasi za mitihani ambazo zimekutwa na makosa na kufutiwa watahiniwa wake, wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya bwawani.  
Waandishi wa habari wakishughudia madudu waliofanya watahiniwa wa kidatu cha nne katika skuli mbalimbali Tanzania, ikiwa ni vielelezo vilivyoletwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dk. Joyce Ndalichoka, kuwaonesha waandishi. 
Waandishi wa habari wakishughudia madudu waliofanya watahiniwa wa kidatu cha nne katika skuli mbalimbali Tanzania, ikiwa ni vielelezo vilivyoletwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dk. Joyce Ndalichoka, kuwaonesha waandishi.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Waandishi na Wakuu wa Chama cha Walimu Zanzibar wakishughudia, baadhi ya vidhibiti vilivyoonekana kufanya kufutiwa matokeo watahiniwa na kidatu cha Nne Tanzania. 
Mdau hata na mimi nilibidi nijionee mwenyewe madudu waliofanya vijana wetu hata kufikia kufutiwa mitihani yao na kupewa adhabu ya kutofanya mitihani kwa muda wa miaka mitatu. 
Mwandishi wa Nipashe Charles Mwakenja, akiuliza swali katika mkutano huo, Baraza lina mpango gani wa kupunguza hiyo adhabu waliotowa kwa Wanafunzi.          
Mwalim Haji na Mwalim Hassan wakifuatilia makaratasi ya mitihani ya Watahiniwa wa kidatu cha Nne, yalioletwa na Katibu Mtendaji waBaraza la Mitihani ikiwa ni vielelezo kuonesha hakuna Mwanafunzi alioonewa katika adhabu hiyo. 
Mwandishi Issa Yussuf, akiuliza swali alitaka kujuwa ni skuli ngapi zilizoshiriki udanganyifu huo wa mitihani.
Mwandishi wa Zanzibar Leo Mwantanga Ame,akiuliza swali katika mkutano huo.   
Kijana Abubakari ameuliza huu ushahidi ulioonesha na kuweza kuwafutia matokeo, na muda wa masaa matatu ya kufanya mitihani inawzekana kuweza kutumika kuwandikia wanafunzi majibu, na baraza litachukuwa hatua gani kwa hawa walimu waliohisika na matatizo haya.yaliofikia kufutiwa matokeo watahiniwa.  
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dk. Ndalichoka, akijibu maswali ya waandishi waliomuuliza, katika mkutano huo uliowashirikisha waandishi wa hwa vyombo mbalimbali vilioko  Zanzibar.

Post a Comment

5 Comments

  1. Ahsante Dr. Ndalichako, naamini umetoa ufafanuzi mzuri na wakutosha.
    Ila, swali linabaki 'wahadimu' watakuelewa?
    Hao, wemkamata ng'ombe mkia, hawawezi kurudi nyuma!

    Mimi, najua tatizo letu kubwa hapa, ni kwamba tunashindwa kua 'objective'..yaani kuliangalia jambo kwa uhalisia wake, mfano, nyeusi tukasema nyeusi na nyeupe tukasema nyeupe!

    Walio wengi Z'bar tayari wanaamini tunaonewa, kwa hivyo hata kama wataoneshwa karatasi zote za matokeo, na namna watoto wetu walivyo kopia hawawezi kuamini!

    Mtoto akichezea 'wembe' mpe ukimkata atajua!
    Mimi naomba hilo baraza la mitihani la Z'bar, lianzishwe tuone unyago wa 'kima' naamini FORM4 watafaulu kama vile FORM 2

    Mwisho wa siku naamini tutakuja lkn. hilo halitokua jambo geni kwa vile sisi tuna historia ya kuishi kwa majuto.

    Mfano mzuri ni wanasiasa wa Z'abar wa miaka ya sitini walivyofanya 'uhafidhina' na sasa wametuachia nakama, sasa na wengine wamehajisomea na kupata vyeti vyao safii kupitia NECTA, wanatafutia wenzao maafa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani unajua baraza la mtihani wanatumia kigezo gani kuamua nani kafaulu na nani hajafaulu? Jee kufaulu ni vipi? Usahihishaji wa mtihani ni tatizo kubwa sana. Kuna uwezekano wanafunzi wengine wakawa wanaonewa katika kufaulu. Zamani tulipokuwa tukienda kusahihisha ilikuwa wanaopitia karatasi za wanafunzi hawaoni majina ya watahiniwa wanadeal na namba tu. Siku hizi wanaopitia mitihani nasikia wanaona mpaka majina kwahiyo wanajua John ni nani na Fatuma ni nani.
      Anyway nakuunga mkono kwa hili la udanganyifu. Ni kweli inasikitisha kuona watu wanawatetea wanafunzi waliofanya udanganyifu. Hivi mlitaka hawa waliofanya udanganyifu waje wawe madaktari wetu? Hebu imagine unatibiwa na mtu mwenye vyeti feki.Waliofanya udanganyifu na waliowasaidiwa ni wahalifu na inabidi washitakiwe.

      Delete
  2. Kaka, naona na wewe wamekupatia (nyaraka)
    Kwa vile unazo naamini,na sisi japo dondoo zitatufikia kupitia.

    ReplyDelete
  3. Hata mimi naomba lianzishwe lakini, uongozi uwe kama ifuatavyo;
    Mwenyekiti: nw.Haji makame ussi
    Kaibu: mw. Shamsi
    Wajumbe: mw. Rabia Nassor Majid.

    ReplyDelete
  4. Anonymous wa pili juu kwa kweli amenipa changamo kdogo!
    Amegusia kua, siku hizi w'funzi badala ya kutumia nambari pekee, wanatumia pia majina yao ktk karatasi za mitihani kwa kweli imenishangaza!

    Naomba jamani, kama kuna mdau wa elimu miongoni mwetu(humu mtandaoni)anijulishe...

    ReplyDelete