Watoto wakiimba wimbo maalum katika sherehe za maafali ya tatu ya kituo hicho.
Watoto wakicheza mchezo wa kuwataka wazazi kuwapeleka watoto katika Vituo vya Maandalizi kwa kujiandaa na Elimu ya Msingi baada ya kutimia miaka saba.
Watoto wakiwa katika mchezo wa mbatata kujaza katika doo, wakikimbia kuwahi kujaza.
Wanafunzi wa Kituo cha Dhin -Noorayni, wakishindana wa Wanafunzi wa Skuli jirani ya Nurulhuda ya Kazole.
Mwanafunzi wa Kituo cha Maandalizi Dhin -Noorayni, fujoni Abdulkadir Haji akisoma risala ya Wanafunzi wakati wa mahafali ya Kituo hicho yaliofanyika Skuli ya Fujoni.
Wanafunzi wakifuatilia matukio mbalimbali ya wanafunzi wezao wakionesha katika sherehe za maafali ya kituo hicho.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi, akiwalisha keki baadhi ya wahitimu wa Kituo hicho katika mahafali ya tatu, tangu kuazishwa mwaka 2009.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Balozi, akitowa nasaha zake kwa Walimu na Wanafunzi wa Kituo hicho katika sherehe za kutimia miaka mitatu iliofanyika katika viwanja vya skuli ya Fujoni.
1 Comments
Lau kama Mashekhe wetu, wangeiewa ayya hii kwa usahihi wake,..wallwahi leo hii tungekua mbali!
ReplyDeleteLkn. wapi?..wanaisoma juu..juu tu bas.
Hawa wanashindwa kweli kwenda huko Uarabuni kuomba msaada wa kusomesha madaktari wa kike ili waweze kutibu wanawake wenzao, badala yake wanakwenda kuomba misaada ya kujenga miskiti!
Hivi unguja hii tuna shida ya miskiti kweli?
Hata wakisomesha kwenye madrassa zao wanashindwa kusisitiza mambo ya elimu ya sayansi.
Utamsikia shekhe" mw'damu anapokufa , aamali zake zote hukatika isipokua swadakatul-jaariyya..
yaani awe amechimba kisima..eti kisima! badala ya kusema shule/hospitali n.k.
Ndio maana leo hii hata mtu akiwa na uwezo wa kiasi gani hapa kwetu atachimba kisima au kujenga msikiti au madrassa.