6/recent/ticker-posts

Matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Uzini Wilaya ya Kati Unguja.

 Maofisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar wakiwa katika Ukumbi Maalum wa  kuhesabia kura kwa jumla vituo vyote hapo Dunga.
Maofisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Wilaya ya Kati, wakisoma matokeo ya Kura kila kituo ili kujumuisha kura zote zilizopigwa atika zoezi la Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Uzini.  
Wagombea wa Uwakilishi Jimbo la Uzini, wakiwa katika Ukumbi wa kuhesabia Kura katika Ofisa za Wilaya ya Dunga, wa kwanza Mgombea wa AFP Rashid Yussuf Mshenga, Salma Hussein Razal CUF.Mohammedraza Hassanali Mohammedali CCM na Ali Mbarouk Mshimba CHADEMA, wakifuatilia jinsi ya ujumlishaji wa kura za kila Kituo uliofanya na Tume ya Uchaguzi.         
Wananchi na Wagombea Uwakilishi wa Jimbo la Uzini, ilibidi wasimame kwa dakika moja kumkumbuka, aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Marehemu Mwalim Mussa aliyefariki kwa ajali ya gari akielekea Bungeni Dodoma mwaka jana. 

Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kati Mussa Ali Juma, akitowa matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Uzini, baada ya kumaliza zoezi la kuhesabu kura katika ukumbi maalum ulioandaliwa na kuwajumuisha Wagombea na Wananchi mbalimbali.
Wagombea wakifuatilia matokea ya kura yakisomwa na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kati Unguja, katika Ukumbi wa Ofisi ya Wilaya ya Dunga.
Wananchi wakiwa katika Chumba cha kutolewa matokea ya kura huko Dunga.
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kati, Mussa Ali Juma, akimkabidhi hati ya ushindi Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza, baada ya kutangazwa matokeo.   
Mshindi wa Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Uzini, kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mohammed Raza, akiwaonesha waandishi na wananchi cheti cha kuthibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo. 


Mgombea wa CHADEMA Ali Mbarouk Mshimba, akitowa shukrani kwa Wananchi waliompigia kura, baada ya kutangazwa mshindi katika ukumbi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kati Dunga.
Mgombea Uwakilishi kwa tiketi ya AFP Rashid Yussuf Mchenga, akitowa shukrani zake kwa Tume na Wananchi wa Jimbo la Uzini  
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia Ushindi wa Mgombea wao baada ya kutangaza matokeo katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Dunga Wilaya ya Kati. Unguja.
Mgombea wa Uwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi Mohammed Raza akishangilia ushindi wake dhidi ya wapizani wake kwa ushindi wa kishindo wa kura 5377.

Post a Comment

0 Comments