KUFUATIA skuli 30 za sekondari kufutiwa matokeo ya kidato cha nne, wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema ndani ya wiki hii, itatoa tamko rasmi juu ya kadhia hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Abdalla Mzee Abdalla, alieleza hayo alipokuwa akizungumza na gazeti hili huko ofisini kwake Mazizini mjini hapa.
Alisema baada ya wizara kukusanya ushahidi ndipo itakapotoa tamko rasmi dhidi ya tatizo hilo la mamia ya wanafunzi wa Zanzibar kufutiwa matokeo yao ya kidato cha nne yaliyotolewa hivi karibuni.
“Tunakusanya maelezo juu ya tatizo hili na ndani ya wiki hii tutatoa tamko rasmi juu ya tatizo hilo”, alisema Naibu huyo.
Naibu huyo alisema kiasi cha skuli 30 zimeathirika kwa kufutiwa matokeo ambapo Chuo cha Kislamu Pemba wanafunzi wote waliofanya mitihani ya kidato cha nne wamefutiwa matokeo yake.
Skuli nyengine ambazo wanafunzi wake wengi wamefutiwa ni Hamamni wanafunzi 158 wamefutiwa matokeo yao, Jang’ombe 117, Regeza Mwendo 79, Filter Federal 79 na skuli ya High View 65.
Akizungumza na gazeti hili mmoja kati ya wanafunzi waliofutiwa matokeo Ummu-lyman Mohammed Ali, kutoka skuli ya Filter Federal alisema wasiadhibiwe wanafunzi juu ya suala la kuvuja mitihani.
Alisema kama mitihani hiyo imefutwa kwa shaka ya kuvuja ni jukumu la wizara ya Elimu kuwaadhibu watumishi wake wenye tamaa ya fedha na kukubali kuvujisha mitihani hiyo.
Mwanafunzi huyo alisema wanafunzi wapewe haki kwa kupewa matokeo yao na wahusika waliovujisha mitihani hiyo kutoka Bara hadi kuvuka maji na kuingia Zanzibar waadhibiwe.
“Huwa tunasikia kila mwaka mtihani hii inavuja kwani wanaovujisha ni nani ni sisi wanafunzi au hao watumishi wabovu wa wizara ya elimu, si vyema kuhukumiwa sisi kwa makosa yao”, alisema.
Hivi karibuni mamia ya wanafunzi wa sekondari wameonesha kufadahaishwa huku wakipanga kufanya maandamo kufuatia kufutiwa matokeo yao ya kidato cha Nne.
2 Comments
See how prof Sheriff analysand this issues
ReplyDeleteDear Salma and the others
I think we are dealing with this question without consideringsome essential issues of rights and responsibilities, and proportionality ofcrime and punishment, and indeed even the Union question comes in.
Salma is trying to convince us that there are some terriblethings that the students have been doing – and I do not doubt it –but obviously there is a distinction between being involved in stealing aquestion paper, and one who does not know the answer who writes Bongo Fleva, orone who uses the opportunity to engage in dirty language. I can see at least 3different issues, and we cannot have a single punishment for all 3.
When I was in Form 2 a classmate of mine used the occasion tohit at British imperialism in 1957 rather than answering questions on Englishliterature, and he was failed; but he was allowed to repeat and passed the followingyear. If this could be done by our British colonial masters, why are we morebrutal than they?
Secondly, even those who did engage in stealing the paper, is athree-year punishment reasonable? To all practical purposes, a student who hasto remain out in the wild for 3 years is finished educationally. It is aneducational death sentence. Why do we want to treat so brutally our ownchildren who made a big mistake, but hopefully will learn the lesson if theyhave to repeat one year.
There is also the question about who is responsible for the examleakage – only the students? not the teachers who are supposed to supervisethe exams? how did the leaked exam papers reach all the way to far-awayvillages in Pemba where children could probably hardly afford to pay the heavy pricefor the leaked papers? Indeed, is not the Baraza la Mitihanio itself the mainculprit for allowing the exams to leak in the first place? Would it not be morejust to send the Baraza la Mitihani packing for 3 years, or even permanentlybecause they are adults who have been given an important responsibility, andfailed?
But then there is the wider question of Zanzibar in the Union. Barazala Mitihani for some reason was made a Union matter among many that were illegitimatelyadded to Union list; but education is not a Union matter. The job of the Barazais to set the exam and mark them, honorably if they can. How did they acquirethe power to determine how the Ministry of Education in Zanzibar wants to dealwith its students who made mistakes and engaged in an unruly way? They are ourchildren, and we have to take care of them in or outside the classroom. Do wein Zanzibar want to increase the gangs of malcontents who will resort to theft,drugs, etc. I say no. Let the mainland deal with the issue their way, but letus not surrender our responsibility to our children’s education or allow thepower of the Zanzibar Government to further diminish. Let this not be yetanother of the never-ending kero za Muungano.
Yours sincerely
Abdul Sheriff
It is very unfortunate that such reckless comment come from a highly respected university professor in the Islands.
ReplyDeleteIt should be noted that forgery in exams is a crime which is punishable in law and that's what the students have commited.
Given the ojective of punishment which is correcting the offender and make him/her not to repeat the crime, I think what NECTA has done is absolutely right.
After all, such punishment is not new and has been around for sometimes, why should it not be applicable now?
The question that teachers also have their part in this crime, doesn't mean that students be let scort free.
Either, NETA was established under Parliamentary Act no.21 of 1973, hence it has the mandate to create it's own bylaws which requires every candidates of the exams to abide with them.
NECTA might not be among the union matters, as the Professor says, but as long as we've accepted to do their exams, their rules should be adhered to, and in case we breach them, we should not expect to be treated differently.
I understand that Mr. sheriff is representing some Z'baris who like to make 'PROBLEM TRANSFER' by moving the blame away from our ministry of education which takes our education for granted and throw all the blame to the union government.