TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemteuwa Dk. Ahmada Hamad Khatib kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kamisheni ya Utalii, Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo Issa Ahmed Othman ndie aliekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambapo sasa amekuwa Mshauri wa Rais wa mambo ya Utalii.
Rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 5(1)(a) cha Sheria ya Kamisheni ya Utalii Namba 7ya 2012
Taarifa iliotolewa na Kaimu Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Salum Maulid Salum imezidi kueleza kuwa Rais pia amemteuwa Shafi Mussa Haji kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme, Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo Mohamed Hashim Ismail ndie aliekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
DKT Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 6(1)(a) cha Sheria ya Shirika la Umeme la Zanzibar.
Uteuzi huo unaanza leo tarehe 5/9/2012
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
5/9/2012
Rais Dkt. Samia Afuturisha Viongozi pamoja na Makundi mbalimbali,
Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu
Hassan akijumuika na Wananchi wa Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba kwenye
Futari aliy...
25 minutes ago
0 Comments