Jahazi ni moja ya Usafiri wa tangu Enzi na Enzi katika mwmbao wa Pwani ya Zanzibar na sehemu nyegine hutumika kama moja ya njia ya usafiri wa sehemu moja hadi nyengine na kutumika sana kusafirishia mizingo mbalimbali wakati wa karne hizo.
Mafundi wa Kijiji cha Nungwi wakiunda Jahazi katika ufukwe wa bahari hiyo, Kijiji cha Nungwi ni maarufu wa uuundaji wa Jahazi tangu enzi hizo na kuwa na mafundi hodari kwa kazi hiyo na kuipatia sifa Zanzibar.
Kama nilivyowakuta mafundi hawa wakiwa katika harakati za kuunda jahazi hilo katika mwambao wa pwani ya nungwi hivi karibuni nikiwa katika matembezi yangu kutembelea vijiji mbalimbali.
0 Comments