Na Laylat Khalfan
WAZEE wameshauri wanafunzi kusomeshwa historia ya nchi yao kabla na baada ya Mapinduzi.Hayo yalielezwa na mshiriki wa kongamano la jumuiya ya wazee wastaafu, wakulima, na wafanyakazi Zanzibar, Haji Seti Haji wakati akichangia kongamano hilo lililofanyika ukumbi wa Baraza la Wakilishi la zamani.
Alisema endapo somo la historia litarejeshwa maskulini litaepusha vijana kutopotoshwa na wanasiasa.
Nae mtoa mada,Dk. Waadili Kavishe,alisema wapo baadhi ya viongozi wanatumia dini kugombanisha watu katika siasa,kwani hakuna hata chama kimoja chenye watu wa dini moja.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Ali Hassan Khamis, alisemataasisi yao itashirikiana na taasisi husika kupiga vita maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
Alisema mabadiliko ya tabianchi yanasababisha athari kubwa kwa uchumi wa wazee.
Aidha aliwataka wanajumuiya hiyo kushirikiana katika kurejesha maadili ya zamani
1 Comments
sina uhakika wazee wetu wanataka historia gani ifundishwe , ikiwa ni suala la kulinda maslahi ya muungano ndio historia basi wamekwenda mchomo hivyo vijipesa kidogo walivyopewa kutumwa kusema yale serikali ya CCM inavyotaka , wakumbuke wao wako zaidi kwa Mola sasa kuliko duniani wasibabaishwa na vizawadi na vipesa vya haramu vya CCM
ReplyDelete