6/recent/ticker-posts

ZSPCA Kutowa Chanjo kwa Mbwa na Paka Zenj.

Na Aboud Mahmoud
LEO ni siku ya kichaa cha Mbwa,ambapo kwa upande wa Zanzibar siku hiyo inaadhimishwa kwa kuwapatia chanjo mbwa pamoja na wanyamna wengine wakiwemo paka.

Kampeni hiyo itafanyika katika kijiji cha Kinyasini mkoa wa kaskazini Unguja.

Katibu wa jumuiya ya kutetea haki za wanyama Zanzibar (ZSPCA), Ali Abdallah Juma alisema mbali ya chanjo pia jamii itapewa elimu kufahamu zaidi madhara yanayotokana na maradhi hayo.

Alisema kauli mbiu ya siku hiyo ni 'kifahamu kichaa cha Mbwa ili tukitokomeze' ambayo inalenga kuwafahamisha wananchi kukielewa zaidi kichaa cha mbwa.

Alisema lengo la kupeleka chanjo hiyo katika kijiji hicho kunatokana na mkoa wa kaskazini Unguja kuongoza kuwa na mbwa wengi wenye kichaa.

Alisema maradhi ya kichaa cha mbwa yanaweza kutoka kwa mnyama na kwenda kwa binaadamu, hivyo ipo haja kwa wananchi kupewa elimu itakayosaidia kujikinga.

Aliwashauri wananchi wanaofuga mbwa au paka kuwapatia chanjo ili kutokomeza maradhi hayo.

Jumuiya ya ZSPCA imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaondosha unyanyasaji wa wanayama na kubahatika kuchaguliwa balozi wa siku ya wanyama duniani kwa upande wa Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments