Na Kauthar Abdalla
MKAAZI wa Bunda mkoani Mara Isaya Keraryo,amemkumbushia Rais Jakaya Mrisho Kikwete juu ya ahadi aliyompa ya kumjengea nyumba ya kuishi.Keraryo ambae ni ana ulemavu alisema, Rais Kikwete alimuahidi kujengea nyumba walipokutana Julai 5, 2010 na kuwaagiza watendaji wake kulishughulikia suala hilo lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, alisema Rais Kikwete alitoa ahadi hiyo kwenye ziara yake katika mkoa huo.
Alifafanua kuwa alikwenda katika mkutano wa Rais akiwa na bango ndipo akampa fursa ya kujieleza naye akamuomba amjengee nyumba kutokana na hali yake alivyo na kwamba watoto na mkewe wanaishi katika mazingira magumu.
Alisema Rais Kikwete alimkubalia ombi lake na kumuagiza Mbunge wa jimbo la Bunda ambae pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Uratibu na Uhusiano, Steven Wasira ahakikishe anasimamia ujenzi wake.
Hata hivyo, alisema Wasira amekuwa kimpiga chenga licha ya kuwa ndie mpiga kura wake.
Alisema maisha magumu ndiyo yanayomsukuma kuzidi kumuomba Rais amjengee nyumba hiyo.
0 Comments