Jhikoman awasha moto Sauti za Busara
Na Andrew Chale, Zanzibar.
MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya Afro
rege, Jhikoman Manyika jana usiku Februari 13, aliwasha
moto kwa kupiga shoo ya nguvu iliyodumu kwa lisaa limoja na kukonga nyoyo
umati mkubwa uliojitokeza kwenye tamasha hilo la 11,la Sauti za Busara mwaka
huu 2014.
Jhikoman alipanda jukwaani majira ya saa
tatu usiku sambamba na bendi yake ya Afikabisa na kupiga vionjo
mbalimbali vya nyimbo zake za sasa na za nyuma.
Jhikoman aliweza kuwasha moto huo kwa
kupiga nyimbo zake zilizopo kwenye albamu yake ya Chikonda na nyingine hali
iliyokonga wadau hao wa muziki wakiwemo wageni kutoka mataifa mbalimbali na
watanzania waliojumukika kwenye tamasha hilo.
Hata hivyo, Jhikoman alisema baada ya shoo
hiyo anatarajia kupiga shoo zingine kwenye nchi mbalimbali kwa kufanya ziara
maalum ikiwemo mataifa ya Ulaya.
Mbali na Jhikoman wasanii wengine ni pmoja
na kundi la Seven Survivor wanopiga muziki wa mchiriku, huku kundi la Baladna
taarabu wao walikonga nyoyo kwa muziki wa mwambao na taarabu asili.
Wengine ni kundi la Pongwa kutoka visiwani
Zanzibar, Tritonik (Motius), na nyingine nyingi.
Awali tamasha hilo lilifunguliwa kwa
paredi iliyokusanya wanamuziki mbalimbali kutoka mataifa yote na kwa kila mmoja
kuonyesha muziki wake mitaani na kasha kumalizikia kwenye viunga vya Ngome
Kongwe.
Aidha tamasha hilo la siku nne,
linatarajiwa kuwa na wanamuziki mbalimbali vikiwemo vikundi 32, vyenye jumla ya
wasanii 200, ambao watapiga shoo kwenye jukwaa hilo la Kimataifa.
Hadi sasa mji wa Zanzibr umebarikiwa kuwa
na wageni mbalimbali wakiwemo waliofika maalum kwa ajili ya shoo na wale
wanaokuja kupumzika kwenye kisiwa hiki cha marashi ya karafuu.
Aidha, tayari idadi ya wageni imeongezeka
huku baadhi ya hoteli zikiwa zimefurika na biashara za kitalii
zikiwa zinanunuliwa kwa wingi.
Kwa upande wake, David Ojoy ambaye ni msaidizi wa masuala ya
habari wa tamasha hilo, anasema kuwa hali ya wageni imekuwa kubwa kufika
kwenye tamasha hilo ikiwemo kupata habari mbali mbali zinazoptikana kwenye
mtandao maalum wa tamasha hilo pamoja vyombo vya habari.
"Tunavipongeza vyombo vya habari kwa kutupa sapoti na
tunaomba tuendelee hivyo hivyo ilikukuza muziki wetu wa kiafrika na kujenga
tamaduni imara hapa afrika na tamasha hili liendelee kuwa la kimataifa
zaidi" alisema Ojay.


0 Comments