
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiashiria jambo wakati wa akiufunga mkutano wa Tafakuri na maridhiano katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania katika ukumbi wa White sand jijini Dar es Salaam,uliowashirikisha wanasiasa,Mashirika ya Kijamii na Viongozi wa Dini mbali mbali nchini.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa siku mbili kuhusu tafakuri na maridhiano katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiufunga mkutano uliowashirikisha watu mbali mbali wakiwemo Wanasiasa,Viongozi wa Dini na Mashirika ya Kijamii Nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania pia Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Joseph Mbatia baada ya kuufunga mkutano wa siku mbili wa Tafakuri na Maridhiano katika kuelekea Katiba mpya ya Tanzania,Ukumbi wa Whitesand Jijini Dar es Salaam leo jioni. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]



0 Comments