6/recent/ticker-posts

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt.Juma Malik Akiwa Katika Ziara Kutembelea Kituo Kidogo cha Kupozea Umeme Welezo


 

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Juma Malik Akili  akiwa pamoja na Waziri wa Maji Nishati na Madini Nadir Abdullatif Alwardi katika Ziara ya kutembelea Kituo Kidogo cha vya kupokea  Umeme Welezo Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Juma Malik Akili kushoto akipatiwa Maelezo na Mkurugenzi wa Kampuni ya ASEEL  Philipe Girad Sariboko kuhusiana na Mradi wa Kituo cha Umeme wa Upepo kinachojengwa katika Eneo la Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
Mitambo ya kupozea Umeme inayojengwa na Kampuni ya SIYUAN ambayo imetembelewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dk Malik Akili pamoja na Waziri wa Maji Nishati na Madini ili kujuwa maendeleo yake Welezo Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Juma Malik Akili akionesha Ishara ya kitu wakati akiwa katika Ziara ya Kutembelea  Eneo la Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme wa Upepo kinachojengwa na Kampuni ya ASEEL katika Eneo la Makunduchi  Mkoa wa Kusini Unguja.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Juma Malik Akili (katikati)akipatiwa Maelezo na Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme (ZECO) Haji Haji wakati alipofanya ziara kuangalia Ujenzi wa Kituo Kidogo cha Kupozea Umeme katika eneo la Welezo Zanzibar .Alie kunja Mikono ni Waziri wa Maji Nishati na Madini Nadir Abdullatif Alwardi.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Juma Malik Akil (wapili kulia)akipatiwa maelezo na Meneja wa Mradi wa Kituo cha kuzalisha Umeme wa Juwa (30 MW) ambacho kinajengwa na Kampuni ya Genereshan Kapital LTD,Kutoka Morishaz Daudi Mwashilindi katika Ziara ya kutembelea Kiituo hicho katika Eneo la Bambi Wilaya ya Kati Zanzibar.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Juma Malik Akili akipatiwa Maelezo na Genereshan Kapital, Stevia Wasira  kuhusiana na hatua ya Maendeleo ya Mradi wa kuzalisha Umeme wa Juwa (30 MW) ambacho kinajengwa na Kampuni ya Genereshan Kapital LTD,atika Eneo la Bambi Wilaya ya Kati Zanzibar.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Juma Malik Akili akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Ziara yake ya kutembelea Ujenzi wa Vituo mbalimbali vya kupokea na kuzalisha Umeme Zanzibar,Kulia mwenyeKofia Nyeupe ni Waziri wa Maji Nishati na Madini Nadir Abdullatif Alwardi.

PICHA NA YUSSUF SIMAI,MAELEZO ZANZIBAR.25/03/2026.

Post a Comment

0 Comments