6/recent/ticker-posts

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amefungua Semina ya Rasimu ya Sheria ya Uinzi wa Taarifa Binafsi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza katika ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo Mawaziri na Naibu Mawaziri kuhusu rasimu ya sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar. 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalenga kuweka Mfumo thabiti wa kisheria utakaosimamia ukusanyaji wa taarifa, matumizi, uhifadhi na ulinzi wa taarifa binafsi.

Yameelezwa hayo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika ufunguzi wa semina ya kiwajengea uwezo Mawaziri na Naibu Mawaziri kuhusu rasimu ya sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Amesema kuwepo kwa Mfumo huo wa kudhibiti wantaarifa binafsi utasaidia  kuziba pengo lililopo sasa la kutokuwepo kwa sheria mahsusi inayodhibiti kikamilifu taarifa binafsi.

Amefahamisha kuwa kutungwa kwa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi ni utekelezaji wa matakwa ya Kikatiba, Kikanda na Kimataifa ambapo katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 15 kinatambua na kulinda haki ya faragha na hifadhi ya maisha binafsi, pamoja na mawasiliano ya kila mtu.

Aidha, Mhe. Hemed ameeleza kuwa   Rasimu ya sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi inalenga kuweka utaratibu wa namna taarifa binafsi zinavyokusanywa, kuhifadhiwa, kutumika pamoja na kuweka wajibu wa Taasisi zote za Umma na Binafsi katika kulinda taarifa binafsi.

Sambamba na hayo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amesema ipo haja ya kushirikiana na mamlaka ya mawasiliano Tanzania  ( TCRA) kutoa semina juu ya matumizi ya vifaa vya electronic pamoja na kulinda haki za wananchi juu ya taarifa zao binafsi na kuweka adhabu kwa yoyote atakaekiuka masharti yaliyowekwa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewaagiza Mawaziri na Naibu Mawaziri kuhakikisha masuala ya ulinzi wa taarifa binafsi yanaingizwa katika Sera, mipango na mifumo ya sekta zao pamoja na kuzingatia usalama wa taarifa katika utendaji wao wa kila siku.

Hata hivyo, amewataka viongozi hao kuhakikisha watumishi wa umma wanapatiwa elimu na miongozo sahihi kuhusu namna ya kushughulikia taarifa za wananchi pamoja na kuwepo kwa ushirikiano mzuri wa  Taasisi za Serikali.

Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano, Technologia ya Habari na Ubunifu Mhe. MUDRIK RAMADHAN SORAGA amesema wizara itazingatia michango iliyotolewa na washiriki wa semina hio ili kuweza kufikia malengo ya utekelezaji wa sheria hio.

Amesema ili kuweza kufikia uchumi wa kigiditali ni lazima kuweka sheria imara, rafiki na wezeshi kwa uwewekezaji ambazo hazitakuwa kikwazo kwao kuja kuekeza Zanzibar.

Mhe.Soraga amesema kwa kuzingatia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050, wizara ya Teknolojia ya Habari imeweka mikakati imara ya uchumi wa kidijitali itakayoweza kuchangia aslimia 10 ya DGP sambamba na kuweka Mifumo mizuri ya ulinzi na usalama kwa wawekezaji.

Wakichangia rasimu hio ya sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi washiriki wa semina hio wamesema ni vyema wizara ikahakikisha sheria hio inazingatia zaidi ulinzi na usalama wa taarifa hasa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa maslahi mapana ya ukuwaji wa uchumi wa Taifa.


Imetolewa na Kitengo cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe 25 /03 / 2026

Post a Comment

0 Comments