6/recent/ticker-posts

Hatimae imekubalika kuwa Paki Darajani.

 Baada ya juhudi kubwa kuchukuliwa na Mdau wa Zanzinews.Com, kuhusiana na eneo hili kukaa bure bila ya kazi yoyote ile na kusababisha eneo la jirani na jumba la treni, kuwa kero kwa watumiaji wa barabara hiyo kwa msongamano wa magari yaliokuwa yakiegesha eneo hilo na kwa watembea kwa miguu. Suala hilo limepatikana ufumbuzi wake kwa kuweka egesho la magari katika eneo lililokuwa kituo cha daladala zamani kufanya maegeshio ya magari na kupungua kwa kiasi kikubwa kero ile na usumbufu wa baadhi ya maderevya kufungiwa magari yao yakiwa yameegeshwa kando ya barabara hiyo. 
Mfanyakazi wa Manispa ya Zanzibar akikatisha tiketi kwa gari linaloegeshwa katika eneo hilo kwa ada ya shilingi 500/= kwa gari moja.

Post a Comment

1 Comments

  1. Mie ninataka parejeshwe asili yake kama awali, pawe ni sehemu ya daladala. Kama sehemu hiyo kwa daladala haitoshi, waifanyie marekebisho kwa kujenga parking complex sio kupafungia. Haiba yote ya mji wa Zanzibar imebadilika na imekuwa vururu vururu tu.

    ReplyDelete