6/recent/ticker-posts

Pamoja Festival Kiruna Sweden

Ujumbe wa wadi za Makunduchi umehudhulia sikukuu ijulikanayo kwa jina la kiswahili "pamoja" yenye lengo la kupiga vita vitendo vya kibaguzi duniani. Mmoja ya wanafunzi wetu waliopo hapa kusoma kwa kipindi cha mwezi mmoja, Nasra Mohamed Mambunga alisoma utenzi wa kiswahili
Siku hii. Utenzi huu ulikuwa na ujumbe wa kuimarisha umoja kati ya watu wa Sweden na Zanzibar. Katika sherehe hii kulikuwa na maonyesho ya bidhaa za Zanzibar kama mikoba, pamoja na tumbuizo za muziki kama vijana hawa wawili wanavyoonekana, Pia kulikuwa na maonyesho ya maisha ya watu wa Makunduchi kwa jumla kwa kupitia kwenye picha. Kwa kweli sherehe ilifanikiwa kuitangaza Zanzibar hapa Kiruna, Sweden
Bidhaa za kazi za mikono kutoka Zanzibar zilivutia watu wengi kwenye sikukuu hii ya Pamoja.


Anisa Mohamed Mambunga kutoka Makunduchi ambaye yupo hapa kwa mafunzo ya mwezi mmoja akighani utenzi wenye ujumbe wa kutoa wito wa kuimarisha zaidi uhusiano kati ya watu wa Zanzibar na watu wa Sweden. Tunaamini uhusiano imara wa nchi ni ule unaowahusisha wananchi wenyewe na sio viongozi. Ndugu Anisa alikuwa kivutio kutokana na umahiri wake wa kuzungumza Kiswedi kwa kipindi kifupi.

Sehemu ya umati uliohudhuria maonyesho ya picha ya maisha ya Watu wa Makunduchi. Aliyevaa koti ni ndugu Kenneth ambaye aliwahi kuwa Meya wa mji wa Kiruna. Hivi sasa ndugu Kenneth ni mwalimu mkuu wa skuli ya Malmfaltens ambayo ndiyo inayohusika na unayosomesha vijana wanaokwenda kufundisha ujasiriamali, kiingereza, kompyuta n.k huko Makunduchi

Post a Comment

0 Comments