Na Kauthar Abdalla
VIONGOZI na
watendaji wa serikali wametakiwa kuongeza nguvu katika kuunga mkono kwa vitendo
kampeni ya safisha Zanzibar
ili kuhakikisha inafikia lengo.
Wakizungumza katika
kampeni hiyo wakaazi wa kijiji cha Nungwi, walisema kufanya hivyo kutaongeza
ari ya utendaji kwa washirika wa maendeleo ambao wameanzisha mpango huo ili
kukuza utalii wa kimazingira.
Mmoja ya wanakijiji
hao, Kazija Silima, alisema endapo hali ya mazingira itakuwa ya kuridhisha idadi
ya watalii wanaotembela kijiji hicho itaongezeka.
Alisema mpango huo
unaoendeshwa na jumuiya ya ZANREC umeanzishwa baada ya Zanzibar
kutangazwa kuwa katika kiwango kisichoridhisha cha usafi ambapo imesababisha
kupokea watalii wa daraja la chini hali inayotishia kuathiri uchumi wa Zanzibar kwa kuwa sekta
ya utalii ndio inayotegemewa.
Alisema kijiji cha
Nungwi kimekuwa kikipokea wageni wengi lakini wanakijiji wanapata hofu ya kupungua kiwango wageni hao kutokana
mazingira yake kutokuwa safi .
Nae Mwenyekiti wa
bodi ya wadhamini wa Jumuiya la Labayka
Development Fund, Haji Khamis Haji, alisema katika kudumisha dhana ya mtu na
mazingira ni vyema kuzingatia madhara ya uchafu ambayo athari yake ni kubwa.
0 Comments