Na Laylat Khalfan
ZAIDI ya shilingi
milioni 300 zimetumika kwa ajili ya mradi wa kuangamiza kunguru weusi kuanzia
2012-2013.
Hayo yalielezwa na
Msaidizi Mratibu wa huo, Salim Ali Khamis, alipokuwa akizungumza na mwandishi
wa habari hizi ofisini kwake Maruhubi.
Alisema mradi huo
unatekelezwa kwa fedha za wafadhili
kutoka serikali ya Finland .
Alisema lengo la
mradi huo ni kupunguza idadi ya kunguru weusi ambao wanasababisha kero na adha
kwa wananchi na maisha ya ndege wengine muhimu.
Alisema kwa kiasi
kikubwa mradi huo umefanikiwa ambapo
kiasi cha kunguru 168,000 wameangamizwa kwa Unguja na Pemba
32,000.
Hata hivyo, alisema
mradi huo unakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo kuibiwa kunguru hao wanapoingia katika mtego.
Aidha alisema kuna
baadhi ya watalii huwa wanawanasua kunguru waliongia kwenye mitego kwa madai
kwamba wanateswa.
Baadhi ya wananchi
wa maeneo ya mjini waliupongeza mradi huo wakisema umesaidia kupunguza idadi ya
kunguru ambao walikuwa kero kwa mifugo yao
ikiwemo kuku.
0 Comments