6/recent/ticker-posts

Waziri Mhe.Shabani ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Vijana na Baraza la Vijana, kutafuta vyanzo vya Ajira ili kuwasaidia Vijana Nchini.

Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe. Shaaban Ali Othaman, amefanya Kikao na Wafanyakazi wa Wizara hiyo katika Ukumbi wa Skuli ya Salim Turkey Mpendae Wilaya ya Mjini.


Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Zanzibar  Mhe. Shaaban Ali Othaman ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Vijana na Baraza la Vijana, kutafuta vyanzo vya Ajira ili kuwasaidia Vijana Nchini.

Mhe. Shaaban ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara hiyo huko Skuli ya Salim Turkey Mpendae Wilaya ya Mjini.


Amesema Ajira zipo nyingi, hivyo ni wajibu wao kuzisimamia ili kuhakikisha zinawafikia Vijana popote walipo Nchini.


Aidha Mhe. Shaaban amewaagiza Wakuu wa Idara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, kusimamia Wafanyakazi wao ili kuongeza uwajibikaji katika Kazi.

 

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Salama Mbarouk Khatib ameahidi kuyasimamia maagizo yaliotolewa kujenga mustakabali nzuri wa Vijana wa Zanzibar.

 

Mbali na hayo, amewataka Wafanyakazi hao, kuongeza juhudi katika kutekeleza majukumu yao ili kufikia azma ya Serikali ya kuwanyanyua Vijana kiuchumi.

 

Nao wafanyakazi wa Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji Zanzibar, wameahidi kuongeza bidii katika kufanyakazi kwa maslahi yao na Taifa kwa Ujumla.

 

                                                        


 

Post a Comment

0 Comments