Na
Mwandishi wetu
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame, amefariki dunia katika hospital ya AMI
Trauma Center, Masaki jijini Dar es
Salaam alipokuwa akitibiwa.
Jaji Makame alifariki dunia baada ya
kuugua maradhi ya moyo kwa muda mrefu.
Alikuwa amelazwa hospitali tangu Julai
mwaka huu hadi mauti yalipomfika alfajiri ya jana.
Julai 28 rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alikwenda kumjulia hali msaafu huyo wa NEC
katika hospitali ya AMI.
Jaji Makame alistaafu NEC tangu Julai
2011.
Mungu aialeze roho ya marehemu
mahali pema peponi,Amina.
0 Comments