Na Mwanajuma Mmanga
Waislamu wanaokwenda Makka
kutekeleza ibada ya Hijja,wametakiwa kutofanya
udanganyifu wakati wanapofanya chanjo za maradhi mabali hasa katika
kipindi hichi ambacho mataifa ya Afrika Magharibi yanapokabiliwa na ugonjwa
hatari wa Ebola.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi, Mkuu wa Shughuli
za Kiislamu, Kamisheni ya Wakfu Mali ya Amana Zanzibar, Khalid Mohammed Mrisho, alisema kutokana na
kushamiri kwa maradhi hayo yanayoambukizwa ni vyema Mahujaji wakawa waaminifu
wanapofanya chanjo.
Alisema kuna uwezekano mkubwa kwa mahujaji ambao wapepitia nchi
zilizoathirika na Ebola kabla ya kuingia Saudi Arababi wakawekwa chini ya
uangalizi maalum, hivyo kuondoa usumbufu chanjo ni muhimu.
Kuhusu viza, alisema kuchelewa
kwa viza zao kunatokana na sababu za kiufundi zilizopo katika ubalozi wa Saudi
Arabia, lakini juhudi zinaendelea kuchukuliwa.
Alisema baada ya kufanya
mazungumzo na ofisi ya ubalozi, wameahidiwa kwamba mtandao huo utakaa sawa
baada ya siku mbili.
“Hadi sasa hakuna Hujaji aliyepata
viza kwa sababu ya kutokea hitilafu za kiufundi,” alisema.
Kundi la mwanzo la mahujaji
litaondoka Septemba 16 kupitia taasisi ya Ahlu Dawa ambao watasafiri kwa ndege
ya shirika la Oman Air.
Kundi la pili litawahusosha
mahujaji wanaosafirishwa na jumuiya za Tawhid, Istiqama, Mother Care, Zanzibar
Hajj na Labaika, ambao wataondoka na
ndege ya Yemen Air Septemba 19.
Alisema na kundi la mwisho linasafirishwa
na Jumuiya ya Al-haramain Septemba
24 mwaka huu kwa ndege ya Shirika la Ndege ya la Yemen
Air.
0 Comments