HAKIMU wa mahakama ya mkoa Chakechake Khamis
Ali Simai, akifungua kongamano la maadhimisho ya siku ya kupinga adhabu ya kifo
duniani, kulia ni mwanasheria wa serikali Ali Hidari na kushoto ni kaimu
Mratibu wa ZLSC Khalifan Amour, ambapo limeandaliwa na kituo cha huduma za
sheria Zanzibar tawi la Pemba na kufanyika ukumbi wa chuo kikuu Zanzibar mjini
Chakechake Pemba (picha na Haji Nassor,
Pemba)
KAIMU Mratibu wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZSLC tawi la Pemba, Khalifan Amour akiahirisha kongamano la siku ya kimataifa ya kupinga adhabu ya kifo, ambapo kongamano hilo lilifanyika ukumbi wa chuo kikuu tawi la Pemba, kulia ni afisa mipango wa kituo hicho Safia Saleh Sultan akifutiwa na mwanasheria wa serikali Ali Hidari (picha na Haji Nassor, Pemba)
BAADHI ya washiriki wa kongamano la kupinga
adhabu ya kifo duniani, lililoandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar
tawi la Pemba, wakimsikiliza mtoa mada mwanasheria wa serikali Ali Haidar,
ambapo kongamano hilo lilifanyika mjini Chake chake (picha na Haji Nassor, Pemba)
1 Comments
Ahsante kwa kutuletea habari za Pemba. The forgotten treasure island.
ReplyDelete