Mkurugenzi wa miradi ya Jamii ya TASAF, Tanzania Amadeus
Kamagenge, akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waalimu, madaktari na wasimamizi
wa miradi ya mfuko huo, kwa walengwa kutoka shehia zilizomo kwenye mpango, yaliofanyika
chuo cha Amali Chakechake, Pemba, kulia ni meneja wa uhaulishaji fedha Omari
Malilo, na kushoto ni kaimu Afisa mdhamini afisi ya makamu wa pili wa rais
Pemba Khadija Khamis Rajab akifutaiwa na afisa mdhamini fedha Bakar Haji.
Afisa habari
wa TASAF makao makuu Dar- es Saalam Zuhura Mdungi akiwasilisha mada namna ya
kujaza fomu za malalamiko kutoka kwa wananchi walengwa, mafunzo hayo
yaliwahusisha waalimu, madaktari na wasimamizi ya miradi hiyo kwenye shehia
zilizomo kwenye mpango kisiwani Pemba
Washiriki wa
mafunzo ya siku mbili juu ya ujazaji fomu maalumu kwa kaya lengwa, ambazo
zinawezeshwa na TASAF, wakimsikiliza Afisa Habari wa TASAF Zuhura Mdungi,
wakati akiwasilisha mada juu ya namna ya kuwasilisha malalamiko na kujaza
kwenye fomu husika, mafunzo hayo yalifanyika jana Chuo cha Amali Vitongoji
Chakechake Pemba
Kaimu Afisa Mdhamini afisi ya makamu wa pili wa rais Pemba Khadija Khamis Rajab,
akifunga mafunzo kwa waalimu, madaktari na wasimamizi wa miradi inayowezeshwa na
TASAF kwenye kaya lengwa, mafunzo hayo yalifanyika chuo cha Amali Vitongoji
Chakechake Pemba(Picha na Haji Nassor Pemba)




0 Comments