THE MWALIMU
NYERERE FOUNDATION
|
India/Makunganya/Bridge
Str.,
P.O. BOX 71000,
DAR ES SALAAM
Fax No: 255 22 2119216/2116040
|
TANZANIA
|
TELEPHONE:
255 22 2118354
255 22 2119216
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)
MDAHALO
WA KUJADILI UMUHIMU WA KUZINGATIA
MAMBO
YA MSINGI KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA
YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
UTAKAOFANYIKA
KWENYE HOTELI YA
BLUE
PEARL, UBUNGO PLAZA DAR ES SALAAM
JUMAPILI
TAREHE 2 NOVEMBA 2014 KUANZIA
SAA
9.00 MCHANA MPAKA SAA 12.00 JIONI
Taasisi
ya Mwalimu Nyerere inapenda kutoa taarifa kwamba imeandaa mdahalo wa Pili wenye
lengo la kujadili umuhimu wa kuielewa
kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba. Mambo
ya msingi yaliyomo katika Katiba hiyo
yataainishwa na kujadiliwa na washiriki
wa Mdahalo. Taasisi ya Mwalimu Nyerere
inapenda kusisitiza kuwa lengo la mdahalo si malumbano au makatazo: Lengo ni
kutoa fursa kwa washiriki wa mdahalo na wananchi kwa ujumla kujielimisha kuhusu
Katiba inayopendekezwa ili waweze kuielewa vizuri, na hivyo kujiandaa kuipigia
kura katika mazingira ya uelewa kwa kuzingatia dhamira yao, bila kulazimishwa,
kutishiwa au hata kulipwa fedha na mtu au kundi lolote. Hakuna kiingilio katika mdahalo huo, na watu
wote wanakaribishwa.
Mdahalo
utafanyika kati ya saa 9.00 mchana na saa 12.00 jioni kwenye Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza,
Dar es Salaam. Washiriki wote wawe
wamefika Blue Pearl Hoteli saa 8 mchana.
2. Washiriki
katika mdahalo huo ni baadhi ya waliokuwa Makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, wakiwamo Mwenyekiti wa Tume Jaji
Joseph S. Warioba, Mzee Joseph W.
Butiku, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bibi Mwantumu
Malale, Mtumishi wa Umma Mwandamizi Mstaafu, , Ndugu Awadh Ali Saidi, Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar
na Ndugu Humphrey Polepole, Mdau wa Maendeleo), Profesa Baregu, Jaji Mstaafu Mzee Ussi
(Zanzibar) na Ndugu Muhammad Mshamba (Zanzibar).wananchi na viongozi kutoka taasisi na asasi
mbalimbali. zinazowakilisha jamii ya Watanzania ambazo ni pamoja na asasi za
kiraia (NGOs), vyama vya siasa, madhehebu ya dini, wasomi, vyombo vya habari,
taasisi za kitaaluma, vyama vya ushirika vya wakulima na wafugaji, vyama vya
wafanyakazi, n.k. wanakaribishwa
kushiriki.
3. Mdahalo
utarushwa moja kwa moja na ITV. Kwa
kupitia TV na Redio zao na TV Sibuka
Maisha. Wananchi popote walipo wanaombwa kushiriki katika
mdahalo huo.
Imetolewa
na:
Mkurugezi
Mtendaji,
Taasisi
ya Mwalimu Nyerere,
S.L.P.
71000,
Fax
No. : 255 22 2119216/2118354
India/Makunganya/Bridge
Street
1
Novemba, 2014
0 Comments