WASHIRIKI wa semina ya siku moja juu ya
mazingatio ya uwezo wa kisiwa cha Pemba kupokea watalii, semina ilioandaliwa na
hoteli ya Manta resort ya Makangaale na Kamisheni ya Utalii, ambapo ilifanyika
ukumbi wa Weni Wete na kufunguliwa na waziri wa habari Zanzibar Mhe: Said Ali
Mbarouk (picha Haji Nassor, Pemba)
MENEJA wa hoteli ya Manta resort ya
Makangaale Micheweni Pemba Mathew Saus, akiwasilisha mada juu uwezo wa kisiwa
cha Pemba kupokea watalii, kwenye semina ilioandaliwa na hoteli hiyo kwa pamoja
na Kamisheni ya Utalii ambayo ilifanyika ukumbi wa mikutano Weni Wete Pemba (picha na Haji Nassor, Pemba)
MKURUGENZI
mkaazi wa ZIPA Pemba, Fadhila Hassan Abdalla akichangia mada juu ya maeneo
yaliotengwa kisiwani Pemba kwa ajili ya utalii, kwenye semina iliofanyika
ukumbi wa mikutano Weni Wete Pemba (picha
na Haji Nassor, Pemba)
WAZIRI wa Habari utamaduni, utalii na
Michezo Zanzibar Mhe: Said Ali Mbarouk akifunga semina ya mazingatio ya uwezo
wa kisiwa cha Pemba kupokea watalii, semina iliofanyika ukumbi wa Weni Wete,
ambayo iliandaliwa na hoteli ya Manta resort na Kamisheni ya Utalii, kulia ni
Kamishina wa Kamisheni ya Utalii Rabia Rashid Abdalla na kushoto na Mwenyekiti wa
kamisheni hiyo dk Ahmada Hamad Khatib (picha
na Haji Nassor, Pemba)
0 Comments