: MWAKILISHI wa Jimbo la Ole wilaya ya
Wete Pemba Mhe: Massoud Hamad Massoud, akizungumza na vijana wa Jimbo lake juu
ya umuhimu wa kupatiwa kitambulisho cha ukaazi cha Zanzibar, wakati mwakilishi
huyo alipokuwa na ziara ya kutembelea zoezi la utoaji wa fomu hizo kwa msheha (picha
na Haji Nassor, Pemba)
KULIA ni Mwakilishi wa Jimbo la Ole Mhe:
Hamad Massoud Hamad akisalimiana na sheha wa shehia ya Ole Mussa Ali Kombo,
wakati mwakilishi huyo alipofanya ziara maalumu ya kuangalia zoezi la ugawaji
wa fomu za kuombea kitambulisho cha ukaazi kwenye Jimbo lake (picha
na Haji Nassor, Pemba)
WAKATI baadhi ya masheha wa Jimbo la Ole wakidaiwa
kukataa kutoa fomu za kuombea kitambulisho cha ZANID, sheha wa shehia ya Ole
Mussa Ali Kombo, amekuwa akigawa fomu hizo kwa wananchi wa shehia yake, kama
alivyokutwa na mpiga picha wetu shehiani humo (picha na Haji Nassor, Pemba)
KULIA ni mwakilishi wa Jimbo la Ole Mhe:
Hamad Massoud Hamad akimuonyesha vyeti vya kuzaliwa sheha wa shehia Mjini Ole
Khamis Shaaban vya wananchi wa shehia wa shehia hiyo, baada ya sheha huyo kudai
hakuna mwananchi mwenye cheti aliekosa fomu za kuombea kitambulisho za ZANID,
wakati mwakilishi huyo alipotembelea zoezi la ugawaji wa fomu hizo jimboni
mwake (picha na Haji Nassor, Pemba)
WANANCHI wa shehia ya Kigongoni Jimbo la
Ole, wakiwa wamesimama kwenye ofisi ya sheha wao majira ya saa 11: 50 jioni
wakimsubiri sheha wao Juma Haji Omar, ili kuwapatia fomu za kuombea
kitambulisho cha ZANID, ambapo baadhi ya masheha jiomboni wamepanga kila Ijumaa
ndio siku ya kutoa fomu hizo (picha na Haji Nassor, Pemba)
MWAKILISHI wa Jimbo la Ole Mhe: Hamad Massoud Hamad akizungumza na waandishi wa habari kwenye shahia ya Minungwini Jimboni humo, mara baada ya kumaliza ziara ya kuangalia zoezi la utaoji wa fomu za kuombea kitambulisho cha ukaazi ZANID (picha na Haji Nassor, Pemba)
0 Comments