6/recent/ticker-posts

Michezo ya Robo Fainali Kuanza Kesho

Kikosi cha timu ya Yanga kinachomenyana na Watoto wa Dago timu ya Shaba ukiku huu katika uwanja wa Amaan hadi sasa timu hizo ziko sare ya bila kufunga ikiwa ni ni kipindi cha pili cha mchezo huo.
Kikosi cha Wazee wa Dogo timu ya Shaba wakionesha kazi katika uwanja wa amaan usiku huu na timu ya Yanga katika mchezo wac mwisho wa makundi Kombe la Mapinduzi 

Michezo ya Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kufanyika kesho katika uwanja wa Amaan kuzikutanisha timu za Simba na Taifa ya Jangombe Wakombozi wa Ngambu. Utafanyika usiku saa mbili katika uwanja wa Amaan.
Michezo ya Robo fainali mingine itafanyika tarehe 8-1-2015 kwa kuzikutanisha timu za KCC ya Uganda na Polisi  jioni saa 9:00 na Saa 11:Jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mtibwa na Azam na Usiku Saa 2:00 kutakuwa na mchezo wa Yanga na JKU michezo yote hiyo itafanyika uwanja  Amaan.. 

Katika mchezo wa kufunga dimba la hatua za makundi unamalizika leo usiku kati ya Yanga na Shaba unaofanyika usiku huu, Timu hizo mpasa sasa bado hazijafungana na sasa ni mapumziko ya kipindi cha kwanza zikiwa sare 

Katika michezo iliofanyika jioni hii katika uwanja wa Mao kulikuwa na Mchezo kati ya Polisi na Taifa ya Jangombe timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.

Mcheo uliofanyika Amaan saa 9:00 jioni kati ya KCC na KMKM, Timu ya KCC kutoka Uganda imeshinda 2--1, ni watetezi wa Kombe la Mapinduzi Mabingwa mwaka jana. wanatetea Kombe lao.

Mchezom uliofanyika jioni saa 11:00 kati ya timu ya Azam na Mtende Rangers timu hizo zimetoka sare ya bila ya kufungana 

Mchezo wa kumalizia usiku huu unaofanyika uwanja wa Amaan kati ya Yanga na Shaba, unaendelea kwa upinzani mkubwa unaooneshwa na vijana wa timu ya Shaba.hizo bado zinaoneshana ufundi wa mchezo.

Post a Comment

0 Comments