6/recent/ticker-posts

Mafunzo ya siku mbili juu ya Uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura la NEC yafanyika Pemba

 MRATIB wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Pemba, Mohamed Ali Jape, akizungumza na maafisa wasaidizi wa Uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura la NEC huko katika ukumbi wa skuli ya Madungu Sekondari kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MAAFISA wa saidizi wa Uwandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura la Taifa NEC kisiwani Pemba, wakimsikiliza kwa makini Katibu Tawala Mkoa wa Kusini Pemba, Ahmed Khalid hayupo pichani wakati alipokuwa akifungua mafuzo ya siku mbili kwa maafisa hao, huko katika Ukumbi wa Skuli ya Madungu Sekondari kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 KATIBU tawala Mkoa wa kusini Pemba Ahmed Khalid akifungua mafunzo ya siku mbili, kwa maafisa wasaidizi wa Uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapigakura la Tiafa NEC, huko katika skuli ya madungu Sekondari Kisiwani Pemba, huku akiwa na watendaji mbali mbali wa Tume hiyo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 AFISA uwandikishaji wa NEC Wilaya ya Chake Chake Kamaria Nassir Ahmed, akizungumza na maafisa wasaidizi wa Uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapigakura la Taifa NEC, huko katika skuli ya Madungu Sekondari chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 AFISA Tehama msaidizi Sajira Mubaga akiwagawia fomu za kiapo, maafisa wasaidizi wa Uwandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura la taifa NEC, huko katika skuli ya Madungu Sekondari Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 KATIBU tawala Mkoa wa Kusini Pemba Ahmed Khalid mwenye suti katikati, akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutoka Tanzania Bara, pamoja na maafisa wasaidizi uandikashaji wa Daftari la kudumu la wapigakura la Taifa NEC, huko katika skuli ya Madungu Sekondari Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MAAFISA wasaidizi wa Uwandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura la Taifa NEC kisiwani Pemba, wakila Viapo cha utendaji wa kazi zao na kutunza siri za Tume katika kipindi cha Uandikishaji, huko katika Ukumbi wa Skuli ya Madungu Sekondari kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)


Post a Comment

0 Comments