6/recent/ticker-posts

JOVAGO kufanya ‘booking’ za hoteli kwa mtandao

Na Kauthar Abdalla
KAMPUNI ya JOVAGO imefungua inakusudua kuanzisha mipango ya kuweza kukodi hoteli ‘hotel booking’, kwa wageni kupitia njia ya mtandao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi ya umoja wa walemavu Zanzibar, ofisa Uhusiano wa JOVAGO, Lilian Kisasa alisema kampuni hiyo itarahisisha upatikanaji wa hoteli kwa njia ya mtandao popote alipo mgeni.

Kisasa alisema huduma hiyo haitoshajihisha hoteli pekee bali pia itashajihisha kukuza utalii kwa sababu itakuwa ni rahisi kwa mgeni anapokwenda sehemu kupata pahali pa uhakika pa kukaa kwa ajili ya shughuli zake.

Aidha alisema kwa sasa soko la mitandao liko wazi kutokana na mahitaji muhimu ya watu ambayo wanatumia kila siku.

Pia alisema kwa sasa kuna hoteli zaidi ya 1,000 Tanzania nzima ambazo wanazitumia kuweka ‘booking’ kwa ajili ya wageni mbali mbali wanaokuja.

Hata hivyo alisema soko la utalii litakuwa kubwa  kwa sababu Tanzania  nzima sehemu ambayo imeendelea kwa kuwa na idadi kubwa ya vivutio ni Zanzibar ambapo pia kati ya hoteli zilizopo 160 zote zipo Zanzibar.

Sambamba na hayo alisema dunia  imebadilika kiasi ambacho wamiliki wa hoteli wanaangalia kukua kwa soko na utandawazi.

Alifahamisha kuwa kampuni ya JOVAGO inalenga kuwafanya Watanzania waelewe utalii wa ndani sio wageni pekee ambao wanaweza kuwa watalii ambapo kwa sasa amesema takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha kufanya boking kimepungua kutokana na harakati za uchaguzi zilizopo nchini.



Post a Comment

0 Comments