Na Masaanja Mabula –Pemba .
VYAMA viwili vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) wadi ya Msuka Jimbo la Konde CUF na NCCR Mageuzi vimeshindwa kukubaliana ni chama kipi kisimamishe mgombea wa Udiwani katika wadi hiyo .
Tayari vyama hivyo kila kimoja kimesimisha mgombea wa anafasi hiyo jambo ambalo limekuwa gunzo katika wadi hiyo juu ya makubaliano yaliyaofikiwa na viongozi wa Juu wa vyama hivyo ambao walikubaliana kugawana nafasi za wagombea .
Chama Cha Wananchi (CUF) chenyewe kimemsimamisha Khamis Ali wakati NCCR Mageuzi wamemsimamisha Mjawiri Rashid na tayari wote wameanza kampeni kuomba ridhaa ya wananchi ili wawachague kushika nafasi hiyo.
Aidha Mjawiri amesema kuwa atawashangaa sana wanachi wa wadi hiyo iwapo hawatamchagua kuwa diwani na kuongeza kwamba yeye ndiye anayefaa kuwakilisha UKAWA na si mwengine na kuwataka wananchi kutofanya kosa na kuchagua kiongozi mwengine .
“Mimi ndiye ninastahili kuwa mgombea wa UKAWA katika wadi hii hivyo nawaomba wananchi msifanye kosa la kuchagua diwani mwengine kwani tulikubalianaa kugawana nafasi za wagombea ”alisema Mjawiri.
Akinadi sera zake Mjawiri ameahidi kuboresha huduma za kijamii kwa kuhakikisha kwamba vijana wote ambao hawana vyeti vya kuzaliwa wanapatiwa pamoja na akuboresha sekta ya michezo ,uvuvi na kilimo kwa kuwahuzalisha ajaira kwa wingi .
Amefahamisha kwamba katika akufanikisha mipango hiyo , iwapo wananchi watamchagua kuwa diwani wa wadi hiyo ataunda kamati ya watu kumi na mbili ambayo ittakuwa na jukumu la kufuatlia kero na changamoto zinazowakabili wananchi ndani ya wadi hiyo.
Pia Mjawiri ameeleza kwamba kamati itaundwa na watu wenye fani tofauti wakiwemo wasomi , wakulima , wavauvi pamoja na wawakilishi wa watu wenye mahitaji maalumuwakiwemo walemaavu , vijana na viongzi wa dini .
“Najua zipo kero nyingi ndani wa wadi hii ikiwemo suala vyeti vya kuzaliwa hilo niko ndani yauwezo wanguna katika kaufanikisha hilo mitaunda kamati ya watu kumi na mbili ambayo itajumauisha wajumbe kutoka avyama vyote vya siasa pamoja na watu maarufu ”alifahamisha .
Mjawiri ambaye pia ni Katibu wa NCCRMageuzi Jimbo la Konde amewashangaa wananchi kushindwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa kampeni na kufahamisha kwamba Kila mwanachama wa CUF , CHADEMA , NCCR Mageuzi na NLD walipaswa kufika katika mkutano huo ili kudhihirisha umoja wao .
Huo ni mkutano wa kwanza kwa Mgombea huyo kuufanya katika shehia ya Makangale ambapo baadhi ya wanachama wa NCCR Mageuzi walitupa lawama kwa wanachama wa vyama vyengine vinavyounda UKAWAkwa kushindwa kuunga mkono katika mkutano huo
0 Comments