MKALIMANI wa Lugha za alama kisiwani Pemba Asha Issa
Mohamed, akiwatafsiria watu wenye ulemavu wa kusikia na kusema, katika
mdahalo wa siku moja, ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa watu wenye
Ulemavu kisiwani Pemba.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
MDHAMINI wa Tume ya Uchaguzi kisiwani Pemba, Ali
Mohamed Dadi akizungumza na watu wenye ulamavu wa kusikia na kusema, katika
mdahalo wa siku moja kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwa watu wenye ulemavu,
mdahalo huo umefanyika Katika Skuli ya Madungu Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
AFISA Elimu kwa wapiga kura Tume ya Uchaguzi
Zanzibar Juma Sanifu Sheha, akiwasilisha mada kwenye mdahalo wa siku moja kwa
watu wenye Ulemavu wa kusinia na kusema, huko katika Ukumbi wa Madungu
Sekondari Chake Chake Pemba.(Picha na
Abdi Suleiman, PEMBA.)
WATU wenye Ulemavu Kisiwani Pemba, wakiangalia mfano
wa karatasi ya kupigia kura, wakati wa mdahalo wa siku moja kwa ulioandaliwa na
tume ya Uchaguzi Zanzibar, huko katika skuli ya Madungu Sekondari Chake Chake
Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKALIMANI wa Lugha za alama kisiwani Pemba Asha Issa
Mohamed akiwaonyesha watu wenye ulemavu wa kutokusema na kuzungumza mfano wa
karatasi ya kupigia kuwa za urais wa Zanzibar, wakati wa mdahalo wa siku moja
ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar, katika skuli ya Madungu Sekondari.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MSHIRIKI wa kongamano la watu wenyeulemavu kutoka
Umoja wa watu wenyeulamavu Zanzibar ofisi ya Pemba, Hadija Mjaka akiuliza swali
katika mdahalo wa siku moja ulioandaliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar, katika
skuli ya Madungu Sekondari.(Picha na
Abdi Suleiman, PEMBA.)
KAMISHNA wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ayyoub Bakari
akitoa ufafanuzi wa maswali ya watu wenye Ulemavu wa kutokusikia na kusema
wakati wa mdahalo wa siku moja, katika skuli ya sekondari Madungu.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
0 Comments