6/recent/ticker-posts

Ligi Kuu ya Zanzibar Yatimua vumbi Uwanja wa Bweleo Kati ya Mafunzo na JKU Imeshinda 2--1

Ligi Kuu ya Zanzibar imeaza leo kutimua Vumbi katika uwanja wa Mpira Bweleo Wilaya ya Magharibi Unguja baada hya uwanja wa Amani Zanzibar kufungwa kwa kutofanyika kwa michezo yoyote na Uongozi wa Uwanja huo na kuifanya Ligi hiyo kuchezwa katika viwanja vya mchangani leo kwa kuzikutanisha Timu za Mafunzo na JKU. Timu ya JKU imeshinda 2--1.  
Kizaza zaa golini kwa timu ya JKU wakati wa mchezo wao wa fungua dimba la Ligu Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika Uwanja wa Mpira Bweleo Wilaya ya Magharibi Nje ya Mji wa Unguja. Timu ya JKU imeshinda mchezo huo kwa mabao 2--1 dhidi ya Mafunzo mabingwa wa Ligi hiyo.
Golikipa wa timu ya JKU akiokoa mpira golini kwake huku mabeki wake wakiwa tayari kuokoa mpira huo.
Mshambuliaji wa timu ya Mafunzo akipiga mpira golini kwa timu ya JKU.







Golikipa wa timu ya Mafunzo akitoa mpira golini baada ya kufungwa bao la Pili na Timu ya JKU katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Bweleo Unguja nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 
Wachezaji wa Timu ya JKU wakishangilia  bao lao la Pili na la ushinda katika mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Zanzibar mchezo uliofanyika kastika uwanja wa Bweleo Wilaya ya Magharibi Unguja Timu ya Jku imeshinda 2--1.

Post a Comment

0 Comments