MKURUGENZI Idara ya Maendeleo ya
Uvuvi Zanzibar Mussa Aboud Jumbe, akielezea hatua wanazopaswa kufanya wajumbe
wa Kamati tendaji ya PECA, baada ya kuja kwa mradi mpya wa uhifadhi wa uvuvi
SWIOfish, kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WAJUMBE wa Kamati tendaji wa PECA wakiwa
katika kazi za vikundi, ili kuchagua siku ya kufanya utambuzi wa maeneo ya
bahari yenye samaki wa matumbawe kwa ajili ya mradi wa SWIOfish, kwenye mkutano
uliofanyika, ukumbi wa makonyo Wawi Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA Mtambuzi wa ardhi Pemba Mohamed
Salim, akionyesha hati ya kukabidhi mashamba yaliotambuliwa kwa ajili ya kwenda
kwa msajili, ili kisha aweze kutoa hati kwa wamiliki wa mashamba ambayo
yameshatambuliwa, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
MRATIBU wa mradi wa Usimamizi wa uvuvi kusini,
magharibi ya bahari ya Hindi SWIOfish, Ramla Talib Omar akiwasilisha taarifa na
malengo ya mradi huo kwa wajumbe wa kamati tendaji wa PECA, kwenye mkutano
uliofanyika ukumbi wa makonyo Wawi Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WAJUMBE wa Kamati tendaji ya PECA, wakimsikiliza Afisa
Mdhamini Wizara ya mifugo na uvuvi Pemba, Mayasa Hamad Ali, wakati akifungua
mkutano wa kuwasilisha mradi wa usimamizi wa uvuvi SWIOfish, uliofanyika ukumbi
wa mikutano Makonyo Chakechake Pemba, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
WAHITIMU TaSUBa WAHIMIZWA KUILINDA AMANI YA TANZANIA
-
Na MWANDISHI WETU, Bagamoyo
WAHITIMU wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), wamehimizwa
kuilinda amani nchini.
Akizungumza katika Mahafali ya...
0 Comments