Afisa Mdhamini Ofisi
ya Rais Ikulu na Utawala bora Pemba, akizungumza na wafanyakazi wake mara baada
ya kumaliza kazi ya kufanya usafi huko ofisini kwake Kibirinzi Chake Chake
Pemba
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa kusini Pemba, Sheikhan Mohamed Sheikhan akifanya usafi katika hospitali
ya Chake Chake, baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe
Magufuli, kutangaza kuwa ni siku ya Usafi disemba Tisa mwaka huu
Baadhi ya watendaji
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, wakifanya usafi katika wodi ya wagonjwa
wanaume katika hospitali ya Chake Chake Pemba
Baadhiya akina mama
wakiwa na wagonjwa wao nje ya hospitali ya chake chake wakisubiri kuingia
ndani, baada ya kumalizika kwa kazi ya usafi katika hospitali hiyo, unaofanywa
na vikosi vya Ulinzi na usalama Mkoa kusini Pemba.
Wafanyakazi wa Baraza
la mji Chake Chake wakifanya usafi katika ofisi yao, mara baada ya kuitikia
wito wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Mgufuli, kuwa
disemba Tisa ni siku ya usafi tu
Wapiganaji wa Jeshi
la wananchi wa Tanzanzia kisiwani Pemba, wakifanya usafi katika hospitali ya
Chake Chake Pemba, kufuagizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John
Pombe Magufuli, kuwa Disemba Tisa mwaka huu ni siku ya Usafi tu
Baadhiya Vitanda vya
wodi ya wazazi katika hospitali ya Chake Chake Pemba, vikiwa nje kufuatia wodi
hiyo kufanywa usafi na wapiganaji wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kisiwani
Pemba.
Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria Pemba, wakifanya usafi
mbele ya ofisi yao mijini Chake Chake kama walivyokutwa na Mpiga picha.
(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)








0 Comments