6/recent/ticker-posts

Wazazi na Walezi Watakiwa Kuwapelea Skuli za Maandalizi Watoto Wao.

Na Majda Kasid –Maelezo Zaznzibar.
Wazazi na Walezi wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika  kuwapeleka watoto wao waliyofikiwa umri wa miaka minne katika skuli za maandalizi kwa lengo la kuwakuza kielimu.

Hayo yameelezwa na  Mkuu wa Divishen ya Elimu ya  Msingi Zanzibar Ahmed Abdul Majid wakati alipokuwa  akitowa  mafunzo  kwa wazazi katika  Kituo cha Walimu (TC) Kiembe Samaki  juu ya umuhimu wa Elimu ya Maandalizi.  

Amesema  wazazi na walezi  ndio wanao hitajika kufanya bidii kwa  kila  hali kuhakikisha watoto wanawapa  kipaumbele  ili kuhakikisha wanapatiwa  elimu  ya  maandalizi na  kujiandaa na    elimu  ya msingi na sekondari.

Amewataka walimu wanaofundisha Wanafunzi kuanzia Elimu ya Maandalizi hadi Elimu ya Sekondari kutowatolesha ada wanafunzi  kwani  hilo ni agizo lililotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.


Alifahamisha  kwamba  mafunzo  hayo yaliyowashirikisha  Walimu wa skuli  za  maandalizi , Walimu  wa  madrasa , Masheha  pamoja  na  Wazazi  yanalengo la   kutoa elimu kwa jamii .

Nae Mkuu wa Kituo cha Maendeleo ya  awali  ya Makuuzi  ya  watoto (ECD) Muhammed Othman Dau amesema  lengo la  mafunzo hayo ni kuwaandaa  wazazi  wa watoto ili waweze  kuanzishwa skuli  za maandalizi mapema  kuwajengea  mfumo mzuri  wa  masomo  ya   baadae.

Amesema  watoto    wanapopatiwa  elimu ya  maandalaizi  huwajengea mustakabali  mzuri  wa maisha ikiwemo  upeo  wa maadili  mema   pamoja  na kuwa na uwezo wa kubuni  mambo  ambayo yatawakuza kiakili na kielimu.

Mohammed Othman Dau amesema hadi hivi sasa watoto waliofikia umri wa miaka mine wanaoandikiswa skuli za maandalizi imefikia   asilimia 50  na lengo ni kuhakikisha watoto wote  wanapelekwa skuli za maandalizi.

Mmoja  ya  wazazi  walioshiriki  mafunzo  hayo Othman Khamis amesema ni  vyema  wanafunzi  wa  maandalizi  kupatiwa walimu wa  masomo  ya  dini.
                           

Post a Comment

0 Comments