HONGERA FAHAD, HONGERA LUMUMBA
Fahad Rashid Salum mwenye umri wa miaka 20 ni mwanafunzi ambaye ametuletea faraja mpya kwa Skuli ya Lumumba pamoja na Wazanzibari wote baada ya kuweza kuirudisha hadhi ya Skuli hii kwa kupata Division One ya point 3, akiwa na alama "A" katika masomo ya Mathematics, Physics na Chemistry na kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wanafunzi bora kitaifa kwa masomo ya Sayansi.
Mapema hivi karibuni, tarehe 7 Julai 2018 katika mahafali ya Kidato cha sita ya Skuli ya Lumumba , Fahad alizawadiwa kuwa mwanafunzi bora wa masomo ya sayansi, huku akikwapua zawadi ya mwanafunzi bora wa Advance Mathematics na mwanafunzi bora wa Physics.
Kabla ya Kujiunga Lumumba, Fahad alipasi mchepuo kutoka Skuli ya msingi ya Mtopepo mnamo mwaka 2012.
Mwaka 2015, Fahad alitokea mwanafunzi wa pili bora kitaifa kwa Zanzibar kwa wanafunzi wa kidato cha nne ambaye alipata Division One ya point 10.
DKT. MWIGULU: TUENDELEE KUMUOMBEA MHE. LUKUVI
-
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akimfariji, Germina Lukuvi, mjane wa
aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na
Wenye Ulemavu...
50 minutes ago

0 Comments