6/recent/ticker-posts

Mchezo wa Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la NMB Mapinduzi Cup Kati ya Mlandege na Singida Big Star Mchezo Uliyofanyika Uwanja New Amaan Complex Zanzibar Timu ya Singida Imeshinda 3-1

Mshambuliaji wa Timu ya Mlandege Aimar Hafidh Abubakar akimpita beki wa Timu ya Singida Big Star katika mchezo wa ufunguzi wa Michuano ya NMB Mapinduzi Cup 2026, mchezo uliyofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.Timu ya Singida Big Star imeshinda mchezo huo kwa bao 3-1. 


TIMU za Mlandege FC na   Singida Black star  zinakutana katika mchezo wa ufunguzi rasmi wa michuano ya NMB Mapinduzi Cup 2026.

Katika mchezo huo Disemba 28,2025 ambao umeanza saa Moja na dakika 20 usiku huu, umezinduliwa na mgeni rasmi, Mhe. Hamza Hasan Juma ambaye ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili, Sera na Uratibu wa Baraza la Wawakilishi.

Mchezo huo wa ufunguzi timu zote zimeweza kutumia ipasavyo wachezaji wake tegemeo, ambapo dakika 16 ya mchezo Mlandege FC walipata penati, hata hivyo Yusuf Suleiman Haji 'Jusa'  amekosa penati hiyo ambayo Metacha Mnata ameweza kucheza kwa kuipangua.

Mpaka dakika ya 45 ya kwanza ya mchezo huo,  timu zikiienda mapumziko bila kufungana.

Kipindi cha pili mchezo huo ulianza kwa kasi, huku timu zote zikifanya mabadiliko ya wachezaji wake kwa Singida BS kumtoa Deus Kaseke, na upande wa Mlandege kwa kumtoa Yusuf Suleiman 'Jusa'.

Dakika ya 72 na 76 na 90+5 zimeshuhudia Singida BS wakipata magoli ya kuongoza.

Dakika 79 Mlandege wameweza kupata bao la kufuatia machozi, mpaka dakika ya mwisho ya mchezo Singida 3-1 Mlandege.

NMB Mapinduzi Cup 2026 inashirikisha timu 10, zikiwemo Simba SC, Yanga, Azam FC, Singida Black na TRA United za Tanzania Bara, Mlandege, KVZ, Fufuni FC na Muembe Makumbi City za Zanzibar, pamoja na URA ya Uganda inayoshiriki kama timu mwalikwa.

Michuano hiyo itakayofikia tamati Januari 13, 2026 siku moja baada ya Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar, NMB na Kamati ya Mashindano hayo wamesaini mkataba mnono, ambao hata hivyo haujatajwa thamani yake.


 

Post a Comment

0 Comments