Naibu Katibu wa Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji Khalid Masoud Waziri akifungua mkutano wa kuhamasisha wa Vyama vya Ushirika kununua hisa katika Benki ya Ushirika Tanzania katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ,Mazizini Wilaya ya Magharibi B.Unguja.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kuhamasisha wanachama wa Vyama vya Ushirika kununua hisa katika Benki ya Ushirika Tanzania wakimsikiliza Naibu Katibu wa Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji Khalid Masoud Waziri (katikati) huko Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ,Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Mwenyekiti wa Muungano wa Vyama vya Ushirika Zanzibar (CUZA) Suleiman Ame Mbarouk akitoa neno la shukrani Kwa Naibu Katibu wa Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji Khalid Masoud Waziri Wakati akifungua mkutano wa kuhamasisha wanachama wa Vyama vya Ushirika kununua hisa katika Benki ya Ushirika Tanzania huko Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ,Mazizini Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Naibu Katibu wa Wizara ya Vijana Ajira na Uwezeshaji Khalid Masoud Waziri amewataka Viongozi wa Vyama vya Ushirika kuwa na mashirikiano katika uendeshaji wa Vyama vyao ili kuweza kupata mafanikio ya Vyama hivyo
Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kuhamasisha wanachama wa Vyama vya Ushirika kununua hisa katika Benki ya Ushirika Tanzania katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ,Mazizini Wilaya ya Magharibi B.
Amesema iwapo Viongozi wa Vyama vya Ushirika watawasimamia ipasavyo wanachama wanaowaongoza, kutasaidia kufikia malengo waliojipangia katika vyama.
Amefahamisha kuwa, Mipango mizuri na madhubuti katika vyama vya Ushirika, ni nguzo muhimu ya kuleta maendeleo ya vyama hivyo.
Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Zanzibar, Zainab Abdulkadir Hassan amesema kujiunga katika Banki hiyo, Itawasaidia Wanaushirika kuweza kukuza mitaji yao.
Aidha amewaomba kuanzishwa Tawi la Banki ya Ushirika Zanzibar ambayo haitokuwa na Riba ili kuendana na Tamaduni na Silka za Wananchi wa Zanzibar.
Nae Mwenyekiti wa Muungano wa Vyama vya Ushirika Zanzibar (CUZA) Suleiman Ame Mbarouk ameiomba Serikali kuviunga mkono vyama vya Ushirika ili viweza kujiendesha na kufikia malengo waliojipangia.



0 Comments