6/recent/ticker-posts

Wanafunzi Waliohitimu Mafunzo ya Ujasiriamali Kuyatumia Vizuri Mafunzo Hayo Ili Yaweze Kuwaletea Tija.

Waziri wa Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar  Mh. Anna Atanas Paul amekabidhi vyeti Wanafunzi 33 wa Ujasiriamali wa fani mbalimbali ikiwemo Ushoni, Upishi na Upambaji wa Uso huko Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.   

Na.Takdir Suweid 

Waziri wa Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto Mh. Anna Atanath Paul amewataka Wanafunzi waliohitimu mafunzo ya Ujasiriamali kuyatumia vizuri ili yaweze kuwaletea tija.

Ameyasema hayo wakati wa mahafali ya Wanafunzi wa Ujasiriamali wa fani mbalimbali huko Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Amesema hali hiyo, itasaidia Vijana  kujiajiri  na kujipatia kipato jambo ambalo litapelekea kuepukana na hali tegemezi katika familia na jamii kwa ujumla sambamba na kukuza Uchumi wa Nchi.


Aidha amesema, lengo la Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto kutoa mafunzo hayo ni kuwajengea ujuzi vijana ili waweze kujishughulisha na harakati za maisha.

Nae, Katibu Mkuu wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Abeida Rashid Abdallah amewataka Wahitimu hao, kuzifanyia kazi fani walizosomea ili zisijepotea.


Hata hivyo, amewataka kuunga mkono mikakati iliowekwa na Serikali ya kupiga vita vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji sambamaba na utumiaji wa Dawa za kulevya na Bangi.


Kwa upande wake Mwakilishi kutoka UNFPA Ali Haji Hamad amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi.


Mbali na hayo ameahidi kuwa Shirika hilo, litaendelea kushirikiana na Serikali katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo na kijamii.


Mafunzo hayo ya miezi 6 ya ujasiriamali wa Ushoni, Upishi na Upambaji wa Uso, yameandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto chini ya Ufadhili wa Shirikal la UNPA ambapo jumla ya Wanafunzi 33 wamehitimu Mafunzo hayo.




Post a Comment

0 Comments