6/recent/ticker-posts

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Amekutana na Kuzungumza na Balozi wa Urusi Nchini Tanzania

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mhe. Andrey Avestian aliefika Ofisini kwake Vuga Zanzibar kwa ajili ya kufanya mazungumzo yaliyolenga kuimarisha zaidi uhusiano katia ya Zanzibar na Urusi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameshukuru nchi ya  Urusi kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania ikiwemo Zanzibar katika sekta mbali mbali za maendeleo.

Ameyasema hayo wakati alipokutana na Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mhe. Balozi  Andrey Avestian aliyefika Ofisini kwake Vuga kwa ajili ya kumsalimia na kumpongeza juu ya  maendeleo makubwa yaliyopo Zanzibar.

Amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa za kimaendeleo ambayo yameletwa na serikali ya awamu ya Nane ( 8 ) ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya bara bara na mahospitali ambayo husaidia kuimarisha austawi wa maendeleo yawananchi wa zanzibar.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ameipongeza Urusi kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya elimu na utamaduni kwa kuiwezesha lugha ya Kiswahili kutumika katika vyuo vikuu livivyopo nchi humo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemuomba Balozi wa Urusi kuangalia namna bora ya kuendelea kushirikiana katika kukikuza na kukisambaza Kiswahili ndani na nje ya Urusi kupitia vyuo vikuuu, taasisi za taaluma na mashirika mbali mbali jambo ambalo litaimarisha ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Nae Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mhe. Balozi ANDREY AVESTIAN   ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kupiga hatua katika kuwaletea maendeleo wananchi wake kupitia nyanja mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya, miundombinu ya Bara bara, Bandari, usafiri wa Anga na mengineyo.

Amsema Urusi imekuwa mstari wa mbele katika kuitumia na kuitangaza lugha ya Kiswahili katika vyuo mbali mbali nchini humo jambo ambalo linaendelea kuimarisha mahusiano mazuri hasa katika nywanja za utamaduni na michezo.

Imetolewa na Kitengo Cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe  28 / 01 / 2026.

.................................................................................

Post a Comment

0 Comments