6/recent/ticker-posts

Mhe Hemed atoa shukurani maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha miradi yote ya maendeleo inayojengwa nchini hususan miradi ya kimkakati inajengwa kwa viwango vinavyokubalika.

 Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa shukurani kwa viongozi wakuu wa nchi,  waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla kwa kushiriki vyema katika sherehe za maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

 Amesema miradi inayoendelea kujengwa nchini inajengwa kwa viwango vinavyokubalika ambapo katika sherehe za Mapinduzi jumla miradi 110 imefunguliwa na kuwekwa mawe ya msingi Unguja na Pemba iliyogharimu shilingi za Kitanzania Trilioni 1.8 ikiwemo miradi ya Afya, Skuli, Barabara, Uwanja wa mpira wa Gombani Pemba, maji safi na salama pamoja na miradi ianayokuza biashara na uchumi wa nchi na kuimarisha ustawi wa wananchi.

 Mhe. Hemed amesema katika serikali ya awamu ya nane uchumi unaendelea kukuwa na  kuimarika sambamba na huduma za jamii zimezidi kuimarishwa mijini na vijijini ikiwa na utekelezaji kwa vitendo adhma ya kufanyika kwa Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964.

 Amesema katika kuhakikisha wawekazaji wanaendelea kuwekeza Zanzibar serikali inajipanga kutatua changamoto ya umeme Visiwani Zanzibar kwa kuhakikisha kunakuwa  upatikanaji wa umeme wa uhakika jambo litakalochangia kukuwa kwa uchumi na kuongezeka kwa pato la Taifa na watu binafsi.

 Akitolea ufafanuzi juu ya miradi iliyoondolewa katika sherehe za Mapinduzi Mhe. Hemed amesema miradi hiyo imeondolewa kutokana na Halmashauri ya sherehe na maadhimisho ya Kimataifa kutoridhishwa na viwango vya miradi hio na hatu iliyofikia.

 Hata hivyo, Mhe. Hemed amebainisha kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshajipanga kwa michuano  ya AFCON ya mwaka 2027 ambapo maandalizi ya ujenzi wa Uwanja wa Zanzibar Arena unaojengwa Fumba Wilaya ya Magharibu “B” unaendelea vizuri na matarajio ni kutumika katika michuano hio.

 Kwa upande wake waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma ameendelea kuwashukuru waandishi wa habari kwa mashirikiano makubwa waliyoyatoa wakati wa maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi na kuwahidi kuwa Wizara zote na Taasisi za Serikali zitatoa mashirikiano katika kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.

 Imetolewa na kitengo cha Habari ( OMPR )

Post a Comment

0 Comments