Na Ali Abass
Watafiti, Wanafunzi na Wanachi wametakiwa kuwa na utamaduni wa kusoma vitabu ili kuongeza fikra, historia, na kuweza kujifunza mbinu mbali mbali za kimaarifa.
Wito huo huo umetolewa na Mwandishi mashuhuri wa vitabu visiwani Zanzibar na Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Jabir, wakati wa ufunguzi wa kitabu chake kipya cha Uchumi wa Mashamba wakati wa Ukoloni wa Uingereza Zanzibar, ( The Plantation Economy During Protectorate in Zanzibar), uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Vuga, Mkoa wa Mjini Magharib, Unguja.
Balozi Jabir alifahamisha kuwa ufunguzi wa kitabu hicho si furaha tu kwake binafsi bali ni utajiri kwa tafiti za uchumi wa kilimo visiwani Zanzibar, ambapo amewataka watafiti na wanafunzi kukitumia kitabu hicho, ili kufanya tafiti za kilimo zitakazo saidia kuimarisha uchumi wa kilimo Zanzibar.
“kitabu hiki kimefafanuwa kwa kina juu ya atahari za ukoloni kwa uchumi wa kilimo Zanzibar, mfano kilimo cha karafuu wakati wa ukoloni na Soko la karafuu wakati kwa wakati huo” Alisema Balozi Jabir.
Aidha amekishukuru Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa maandalizi mazuri ya uzinduzi wa kitabu hicho, na pia alitoa shukurani zake kwa msimamizi wa kitabu chake, Prof. Abdul Sharif.
Kwaupande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar SUZA, Dkt Saada Omar Wahab, aliwahimiza Wanafunzi wa Chuo hicho kuwa na tabia ya kusoma vitabu ili kuweza kufanikisha wanafanya vizuri katika masomo yao.
Akitoa pongezi kwa Muandishi Msimamizi wa kitabu hicho, Prof. Abdul Sharif alisema, kitabu hicho kimekusanya tafiti za kina kuhusu kilimo, tangu enzi za wakoloni ambapo, kilimo cha karafuu kilishamiri Visiwani Zanzibar.
Uzinduzi wa kitabu hicho ulihudhuriwa na wanafunzi, watafiti, wanahistoria, ndugu jamaa na marifiki, ambapo kitabu hicho kinakusudiwa kubadilisha mfumo wa kilimo nchini,kuwasaidia Walimu, Wanafunzi na watafiti.



0 Comments