Uongozi wa Baraza la Manispaa Magharibi ‘A’ umefanya mazungumzo na Meneja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ili kubadilishana mawazo na kuweka msingi wa ushirikiano wa muda mrefu.
Meneja wa NBC alisema Benki iko tayari kushirikiana na Manispaa katika masuala ya kifedha, ikiwa ni pamoja na kuifanya Manispaa kuwa mteja/mshirika wa Benki, na kuwapa watendaji wake mikopo kwa urahisi na masharti nafuu.
Alisisitiza umuhimu wa kujenga mahusiano imara na taasisi za umma ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuboresha ustawi wa watumishi.
Uongozi wa Manispaa uliishukuru NBC kwa nia hiyo na kueleza kuwa wako tayari kuendeleza mazungumzo na kuikaribisha Benki mara kwa mara Ofisini kwao.
Kikao hicho kimeelezwa kuwa mwanzo mzuri wa uhusiano mwema unaotarajiwa kuleta faida kwa pande zote mbili na kuongeza motisha kwa watendaji wa Manispaa.


0 Comments