Na mwandishi wetu Zanzibar.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Hassan Ali Hassan amewataka Maafisa wa Uhamiaji kuzidisha bidii katika majukumu yao ya kazi kwani ndio msingi wa mafanikio kazini.
Amezungumza hayo mara baada ya kuwavalisha vyeo Maafisa 14 Kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji katika iliyofanyika leo tarehe 09 Februari 2026 Afisi Kuu ya Uhamiaji, Zanzibar.
Akisisitiza uwajibikaji katika kazi Kamishna Hassan amewataka maafisa waliopata vyeo hivyo kuwa ni mfano wa kuigwa kwa nidhamu, uadilifu na kua wazalendo kwa nchi yao.
“Cheo ni heshima hivyo tuipokee kwa kuongeza kasi ya utendaji kazini”, akitilia mkazo suala zima la kufanya kazi kwa kujitolea.
Aidha, Kamishna Hassan alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kupandishwa vyeo
Maafisa Uhamiaji katika ngazi mbalimbali.
Jumla ya Maafisa 64 wa Idara ya Uhamiaji Tanzania wamepandishwa vyeo kwa ngazi
mbalimbali ikiwa ni mkakati wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa kuhakikisha vyombo
hivyo vinafanya kazi kwa bidii na weledi kwa maslahi ya Taifa


0 Comments